-
Russia: Shambulio la droni la Ukraine ni ugaidi wa kimataifa
Jul 24, 2023 11:21Russia imelitaja shambulio la ndege zisizo na rubani (droni) za Ukraine dhidi ya Moscow kuwa ugaidi wa kimataifa.
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia: Marekani inahusika katika uhalifu wa mauaji ya mwandishi habari Mrussia
Jul 24, 2023 11:04Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema Marekani inahusika katika uhalifu mpya wa Ukraine wa mauaji ya mwandishi wa habari wa Russia kwa kutuma mabomu ya vishada nchini Ukraine kwa kisingizio cha vita nchini humo.
-
Russia yatoa masharti saba ya kurudi tena kwenye mkataba wa usafirishaji nafaka
Jul 23, 2023 02:17Russia imetangaza kuwa iko tayari kurejea kwenye na mkataba wa nafaka uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki, lakini kwa sharti tu kwamba mataifa ya Magharibi na Ukraine yatimize wajibu wao wa muda mrefu kuhusiana na Moscow ambao yameshindwa kuutekeleza hadi sasa.
-
Marekani yaona fahari kutumiwa silaha zake haramu za vishada Ukraine
Jul 21, 2023 07:49Marekani imepongeza na kusifu uamuzi wake wa kutuma mabomu yaliyopigwa marufuku kimataifa ya vishada nchini Ukraine.
-
Russia yaruhusu kuanzishwa benki za Kiislamu katika baadhi ya maeneo
Jul 20, 2023 07:20Bunge la Russia (Duma) limeidhinisha muswada wa sheria inayoruhusu kuanzishwa kwa mfumo wa benki za Kiislamu katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.
-
Safari ya John Kerry mjini Beijing: Jitihada za kuzuia ukaribu wa China na Russia
Jul 18, 2023 05:19John Kerry, mwanadiplomasia mkongwe na mwakilishi maalum wa Marekani katika masuala ya tabianchi aliwasili China Jumapili.
-
Ukosoaji mkali wa Putin kwa hatua ya Ulaya ya kuifuata kibubusa Marekani
Jul 18, 2023 02:27Rais Vladimir Putin wa Russia amekosoa vikali kutokuwa huru nchi za Ulaya na kuwa tayari nchi hizo kutekeleza kibubusa amri na maagizo ya Marekani.
-
Russia yasitisha ushiriki wake kwenye makubaliano ya nafaka ya Bahari Nyekundu
Jul 17, 2023 12:09Ikulu ya Kremlin imetangaza kuwa Russia imesitisha ushiriki wake katika makubaliano ya kuruhusu meli ya Ukraine iliyobeba nafaka kuvuka Bahari Nyeusi kuelekea maeneo ya dunia yanayokabiliwa na njaa kwa ajili ya kufikisha bidhaa hiyo, hatua ambayo ni pigo kwa usalama wa chakula duniani, kutokana na ongezeko la bei kufuatia uvamizi wa Moscow dhidi ya Kyiv.
-
Russia yawatahadharisha Wamagharibi kuhusu kutuma mabomu ya vishada huko Ukraine
Jul 17, 2023 04:23Rais wa Russia amezitahadharisha nchi za Magharibi kuhusu kutuma mabomu ya vishada huko Ukraine kwa kisingizio cha vita. Rais Vladimir Putin amebainisha haya kufuatia uamuzi wa karibuni wa Marekani kuhusu kutuma silaha hizo zizilizopigwa marufuku kimataifa huko Ukraine.
-
Sisitizo la Russia la kuheshimu umoja wa ardhi yote ya Iran
Jul 16, 2023 08:04Mikhail Bogdanov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia na mwakilishi maalumu wa rais wa nchi hiyo katika masuala ya Asia Magharibi na Afrika, amesisitiza juu ya kuheshimiwa mamlaka na umoja wa ardhi yote ya Iran kama nchi rafiki. Bogdanov ameyasema hayo katika mkutano na Kazem Jalali, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Moscow.