-
Ayatullah Khatami: Marekani inaongoza duniani kwa kukiuka haki za binadamu
Aug 18, 2017 14:49Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria jinai za kibaguzi nchini Marekani na kusema kuwa, Marekani inaongoza duniani kwa kukiuka haki za binadamu na kwamba, viongozi wa nchi hiyo wanapaswa kuona haya na aibu kuzungumzia suala la haki za binadamu katika nchi nyingine.
-
Khatibu: Makombora ya IRGC yalikuwa jibu muafaka kwa magaidi
Jun 30, 2017 14:15Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran Ayatullah Imami Kashani amesema hatua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, IRGC, kushambulia kwa makombora ngome za magaidi wa ISIS nchini Syria ilikuwa ni jibu muafaka na adhabu kwa magaidi hao wakufurishaji.
-
Kermani: Kushikamana na Uislamu na Qur'an ndio mafanikio ya Iran
Jun 16, 2017 15:27Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo mjini Tehran, Ayatullah Muhammad Ali Muvahhedi Kermani amesema kuwa, Marekani ndiye adui mkuu wa taifa la Iran na kwamba, kushikamana na misingi ya dini ya Uislamu na Qur'an Tukufu ndiko kulikoiwezesha Jamhuri ya Kiislamu kusimama imara mbele ya Marekani na maadui wengine.
-
Alaeddin Boroujerdi: Marekani ni mpangaji mkuu wa njama dhidi ya Iran
Jun 10, 2017 03:57Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria mashambulio ya kigaidi ya siku ya Jumatano hapa mjini Tehran na kusema kuwa, hapana shaka kuwa, mpangaji mkuu wa njama hiyo ni Marekani mtenda jinai.
-
Sala ya kwanza ya Ijumaa Mwezi wa Ramadhani katika Msikiti wa Al Aqsa
Jun 02, 2017 14:22Maelfu ya Wapalestina wameshiriki katika sala ya Ijumaa ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika Msikiti wa Al Aqsa kwenye mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel huku ya wanajeshi wa utawala huo wa Kizayuni wakiwa wameweka sheria kali za kuwabana Waislamu.
-
Ayatullah Khatami: Bahrain imegeuzwa kuwa jela kubwa ya wananchi
May 26, 2017 14:01Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran sambamba na kulaani hujuma na uvamizi wa vikosi vya usalama vya Bahrain dhidi ya nyumba ya Sheikh Issa Qassim mwanazuoni mashuhuri wa nchi hiyo ametangaza kuwa, utawala wa Aal khalifa kwa kufanya ukandamizaji, kamatakamata na aina mbalimbali za jinai, umeigeuza nchi hiyo na kuwa jela kubwa kwa ajili ya wananchi.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Mahudhurio makubwa ya wananchi katika uchaguzi yatadhihirisha nguvu ya Iran
Apr 21, 2017 16:23Khatibu wa Swala ya Ijumaa katika mji wa Tehran amesema kuwa kushiriki kwa wingi wananchi wa Iran katika uchaguzi ujao, kutaonyesha nguvu na uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Ayatullah Siddiqi: Hujuma ya Marekani huko Syria, ni kinyume cha sheria za kimataifa
Apr 14, 2017 15:05Khatibu wa Sala ya Ijumaa katika mji wa Tehran amesema kuwa, shambulizi la Marekani nchini Syria siku ya Ijumaa iliyopita, linakinzana na sheria zote za kimataifa.
-
Ayatullah Kashani: Waungaji mkono wa magaidi, ndio waliotekeleza mashambulizi ya kemikali huko Syria
Apr 07, 2017 13:02Imamu wa Muda wa Sala ya Ijumaa hapa Tehran amesema kuwa Marekani na waungaji mkono wa magaidi katika eneo wanayapatia silaha na mada za kemikali makundi ya kigaidi huko Syria.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran awataka wananchi kushiriki kwa wingi katika uchaguzi ujao
Mar 24, 2017 16:24Imamu wa Muda wa Swala ya Ijumaa hapa Tehran amesisitiza udharura wa wananchi kushiriki kwa wingi katika uchaguzi ujao wa Rais na mabaraza ya miji ya vijiji uliopangwa kufanyika tarehe 19 mwezi Mei mwaka huu na kueleza kuwa, kushiriki idadi kubwa ya wananchi katika uchaguzi ujao kutaimarisha utambulisho wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.