Ayatullah Khatami: Marekani inaongoza duniani kwa kukiuka haki za binadamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i33308-ayatullah_khatami_marekani_inaongoza_duniani_kwa_kukiuka_haki_za_binadamu
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria jinai za kibaguzi nchini Marekani na kusema kuwa, Marekani inaongoza duniani kwa kukiuka haki za binadamu na kwamba, viongozi wa nchi hiyo wanapaswa kuona haya na aibu kuzungumzia suala la haki za binadamu katika nchi nyingine.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 18, 2017 14:49 UTC
  • Ayatullah Khatami: Marekani inaongoza duniani kwa kukiuka haki za binadamu

Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria jinai za kibaguzi nchini Marekani na kusema kuwa, Marekani inaongoza duniani kwa kukiuka haki za binadamu na kwamba, viongozi wa nchi hiyo wanapaswa kuona haya na aibu kuzungumzia suala la haki za binadamu katika nchi nyingine.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo leo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kubainisha kwamba, hatua alizochukua Rais Donald Trump wa Marekani zinaunga mkono jinai za kibaguzi.

Katika maandamano ya kupinga ubaguzi yaliyojiri siku ya Jumamosi iliyopita katika mji wa Charlottesville kwenye jimbo la Virginia, kijana mmoja wa kundi linalolingania ubaguzi aliushambulia kwa gari mkusanyiko wa watu waliokuwa wanaandamana kupinga vitendo hivyo na kuua mwanamke mmoja na kujeruhi watu wengine 19.

Ayatullah Ahmad Khatami, Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran

Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amelaani vikali pia jinai za makundi ya kigaidi katika kijiji cha Mirza Olang nchini Afghanistan na Barcelona nchini Uhispania na kueleza kuwa, makundi ya kigaidi likiwemo la Daesh yameanzishwa na kulelewa na Marekani na kwamba, ili wananchi wa madola ya Magharibi waweze kuondokana na jinai za magaidi wanapaswa kuwataka viongozi wa nchi zao waache kuyaunga mkono makundi ya kigaidi.

Ayatullah Ahmad Khatami ameashiria pia mjadala wa wa Bunge wa kuchunguza ustahiki wa majina ya mawaziri waliopendekezwa na Rais Hassan Rouhani katika serikali yake ijayo na kubainisha kwamba, awamu ya kumi na mbili ya serikali ya Iran inapaswa kutumia uwezo wake wote kwa ajili ya kutoa huduma kwa dini, maanawi, madili na wananchi.