-
Qatar yataka Saudia na Imarati zitimuliwe Baraza la Haki za Binaadamu
Jun 23, 2018 09:42Baada ya kupita mwaka mmoja tangu kukatwa mahusiano ya nchi za Kiarabu na Qatar na kadhalika kuiwekea vikwazo na mzingiro wa kila upande nchi hiyo, serikali ya Doha imetaka uanachama wa Saudia na Imarati katika Baraza la Haki za Binaadamu usimamishwe.
-
Syria: Riyadh ingali inawazuia raia wetu kwenda kufanya Hija
Jun 23, 2018 02:55Serikali ya Syria imeukosoa vikali utawala wa Aal-Saud kwa kuingiza siasa katika amali tukufu ya Hija, ambapo Riyadh imewazuia raia wa Syria kwenda kutekeleza ibada hiyo kwa mwaka wa saba mfululizo.
-
Jumuiya ya Maimamu Tunisia: Saudia inatumia mapato ya Hija kushambulia nchi za Waislamu
Jun 21, 2018 23:16Jumuiya ya Maimamu wa Swala za Jamaa nchini Tunisia imetoa taarifa ikisisitiza kuwa Saudi Arabia inatumia mapato yanayotokana na ibada ya Hija kwa ajili ya kuzishambulia nchi nyingine za Kiislamu na imemtaka Mufti Mkuu wa nchi hiyo kusimamisha safari za kwenda kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu huko Saudia.
-
Ndege za Saudia zadondosha mabomu Hudaydah Yemen wakati wa Sala ya Idul Fitri
Jun 15, 2018 10:59Ndege za kivita za muungano unaoongozwa na Saudia zimedondosha mabomu katika maeneo ya mji wa bandarini ya Hudaydah nchini Yemen wakati wakaazi wa mji huo wakiwa wamekusanyika kwa ajili ya Sala ya Idul Fitr mapema leo asubuhi.
-
Saudia yadondosha mabomu katika kituo cha tiba nchini Yemen
Jun 12, 2018 09:14Ndege za kivita za Saudi Arabia zimedondosha mabomu katika kituo kimoja cha afya cha kuwatibu watu wenye kipindupindu nchini Yemen ambacho kinasimamiwa na Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF).
-
Ripoti: Saudia inafanya mipango ya kumrejesha madarakani dikteta wa zamani wa Tunisia
Jun 12, 2018 02:03Chombo kimoja cha habari nchini Tunisia kimefichua kuwa Saudi Arabia inafanya njama za kumrejesha madarakani dikteta wa zamani wa nchi hiyo.
-
Meja Jenerali Soleimani: Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imebadilika kuwa serikali ya Muqawama
Jun 11, 2018 23:47Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema: Saudi Arabia imetumia katika muda mfupi tu dola milioni 200 kwa ajili ya uchaguzi wa bunge la Lebanon, lakini harakati ya Hizbullah ndiyo iliyoibuka mshindi katika uchaguzi huo.
-
Ripoti: Saudia na Imarati zinapanga kufanya mapinduzi Bahrain
Jun 09, 2018 03:39Tovuti ya habari ya Middle East Eye imeripoti kuwa, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zinapanga njama ya kumuondoa mamlakani Waziri Mkuu wa Bahrain, Khalifa bin Salman Aal-Khalifah.
-
Qatar: Saudia iache kuingiza masuala ya dini katika mgogoro wa kisiasa
Jun 06, 2018 09:50Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu nchini Qatar sambamba na kuelezea mwenendo wa vizuizi vinavyofanywa na Saudia kwa ajili ya kuwazuia raia wa nchi hiyo kuweza kushiriki ibada ya hija, imeitaka Riyadh kuacha kuyaingiza masuala ya kidini katika mgogoro wa kisiasa wa pande mbili.
-
Mwaka mmoja wa mgogoro kati ya nchi za Kiarabu
Jun 06, 2018 01:27Umetimia mwaka mmoja tokea uanze mgogoro baina ya nchi za Kiarabu na dalili zote zinaonyesha kuwa mgogoro huo ungali unaendelea bali hata utazidi kupanuka na kuwa mbaya zaidi.