Ripoti: Saudia na Imarati zinapanga kufanya mapinduzi Bahrain
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i45614-ripoti_saudia_na_imarati_zinapanga_kufanya_mapinduzi_bahrain
Tovuti ya habari ya Middle East Eye imeripoti kuwa, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zinapanga njama ya kumuondoa mamlakani Waziri Mkuu wa Bahrain, Khalifa bin Salman Aal-Khalifah.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 09, 2018 03:39 UTC
  • Ripoti: Saudia na Imarati zinapanga kufanya mapinduzi Bahrain

Tovuti ya habari ya Middle East Eye imeripoti kuwa, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zinapanga njama ya kumuondoa mamlakani Waziri Mkuu wa Bahrain, Khalifa bin Salman Aal-Khalifah.

Duru za kidiplomasia zimeiambia tovuti hiyo ya habari kuwa, lengo la Saudia na Imarati kumuondoa madarakani Bin Salman Aal-Khalifa ambaye ndiye Waziri Mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi duniani, ni kuimarisha ushawishi wao katika nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.

Duru hizo za kidiplomasia zimebainisha kuwa, katika hali ambayo viongozi wazee katika eneo wanamuunga mkono Khalifa, lakini viongozi vijana wakiwemo Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia, Mohammed bin Salman na Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Abu Dhabi, Mohammed bin Zayed Al Nahyan wanamuunga mkono Mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Aal-Khalifah kumuweka pembeni Waziri Mkuu wa Bahrain.

Wakati huo huo, gazeti la al-Quds al-Arabi lenye makao yake mjini London limedokeza kuwa, kuna mgogoro mkubwa ndani ya utawala wa Aal-Khalifa, na kwamba Mfalme wa Baharain ameazimia kumuengua madarakani Waziri Mkuu wa nchi hiyo baada ya uchaguzi wa bunge baadaye mwaka huu.  

Mfalme wa Bahrain

Tangu mwaka 2014 Februari 2011, Bahrain imekuwa ikishuhudia mwamko wa wananchi dhidi ya utawala wa kiimla na kidikteta wa Aal-Khalifa ambapo Wabahrain wanadai uhuru, kuimarishwa uadilifu, kuondolewa ubaguzi na kuingia madarakani utawala uliochaguliwa na wananchi.

Hata hivyo utawala wa Aal-Khalifa badala ya kujibu malalamiko hayo ya wananchi, umekuwa ukitumia ukandamizaji wa kila namna kuzima malalamiko hayo.