-
Iran yaipongeza Iraq kwa kushajiisha mazungumzo katika eneo
Jul 18, 2022 03:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameipongeza Iraq kwa nafasi yake athirifu na jitihada zake za kushajiisha utumiaji wa mazungumzo kwa ajili ya kujaribu kutatua matatizo na changamoto zinaolikabili eneo hili la Asia Magharibi.
-
Hizbullah yatoa msimamo kwa hatua ya Saudia kuifungulia Israel anga yake
Jul 17, 2022 06:28Hizbullah ya Lebanon imesema, hatua ya Saudi Arabia ya kuufungulia utawala haramu wa Kizayuni wa Israel mipaka ya anga yake ni sawa na kuwa mshirika wa jinai zinazofanywa na utawala huo na ni usaliti kwa umma wa Kiislamu.
-
Hamas yapinga misimamo ya Saudia ya kujikurubisha zaidi kwa wazayuni maghasibu
Jul 15, 2022 22:25Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imepinga vikali hatua ya Saudi Arabia ya kufungua anga ya nchi hiyo kwa ndege za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Ndege maalumu ya shirika la ujasusi la Israel, Mossad yatua Riyadh, Saudi Arabia
Jul 11, 2022 22:50Vyombo vya habari vya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel vimeripoti kuwa, ndege maalumu ya shirika la ujasusi la utawala huo Mossad imetua katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.
-
Jaribio la Biden kuhalalisha safari yake ya Saudi Arabia
Jul 11, 2022 20:55Rais Joe Biden wa Marekani amedai katika makala iliyochapishwa kwenye gazeti la Washington Post kwamba katika kipindi cha miezi 18 ya uongozi wake, eneo la Asia Magharibi limekuwa shwari na salama zaidi kuliko hapo awali. Biden ameyasema hayo katika jitihada zake za kujaribu kuhalalisha safari yake tarajiwa nchini Saud Arabia.
-
Mapendekezo ya Amnesty International kwa Riyadh kuhusu haki za binadamu
Jul 11, 2022 03:51Shirika la Kutetea Haki za Binadamu lisilo la kiserikali la (Amnesty International) limetaka kusainiwa waraka ambao unamtaka Mfalme wa Salman wa Saudi Arabia aondoe marufuku ya kiholela dhidi ya safari ya wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu nchini humo.
-
Saudia inakaribia kuwanyonga vijana watano raia wa nchi hiyo
Jul 03, 2022 23:02Utawala wa Aal Saud unaendelea kutekeleza vitendo vyake viovu na vilivyo kinyume cha sheria kwa kuwafunga jela raia kinyume cha sheria kutokana na umri wao mdogo, kwa tuhuma zisizo na msingi.
-
Iran yakamilisha oparesheni ya kuwatuma waumini kwenda Hija
Jul 03, 2022 04:54Mkuu wa oparesheni ya kuwabeba Wairani wanaoenda kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu amesema oparesheni hiyo inakamilika usiku wa leo.
-
Njama mpya za Marekani na Saudi Arabia nchini Syria
Jun 25, 2022 22:02Baadhi ya vyanzo vya habari vimeripoti kuwa Marekani na Saudi Arabia zimeanzisha jitihada za pamoja za kuunda upya kikosi kinachojulikana kwa jina la Jaish Maghawir al-Thawra (Jeshi la Makomando wa Mapinduzi) katika kituo cha Al-Tanf kinachosimamiwa na Marekani kilichoko kwenye mpaka wa Jordan, Syrian na Iraq.
-
Iran yatuma ujumbe wa watu sita katika ubalozi wake mdogo nchini Saudia
May 31, 2022 03:08Iran imetuma wajumbe wake sita wa ubalozi mdogo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje kwa ajili ya kwenda kutoa huduma kwa raia wa Iran wakati wa ibada za Hija mwaka huu.