Mapendekezo ya Amnesty International kwa Riyadh kuhusu haki za binadamu
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu lisilo la kiserikali la (Amnesty International) limetaka kusainiwa waraka ambao unamtaka Mfalme wa Salman wa Saudi Arabia aondoe marufuku ya kiholela dhidi ya safari ya wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu nchini humo.
Shirika la Amnesty International limetangaza kuwa, wakati familia mbalimbali zikisherehekea Sikukuu ya Idul Adh'ha; Saudi Arabia inawatenganisha ndugu wa wanaharakti hao kwa kustafidi na mafuruku yake hiyo ya kiholela dhidi ya wanaharakti na watetezi wa haki za binadamu.
Amnesty International imeongeza kuwa, katika miaka ya karibuni jamii ya Wasaudi imeshuhudia hatua za aina yake zikichukuliwa ili kuboresha hali ya kijamii lakini kinyume na mafanikio hayo makubwa, kuna ukweli unaodhihirisha kuwepo ukandamizaji mkubwa na endelevu dhidi ya makumi ya watetezi na wanaharakati wa haki za binadamu nchini Saudia. Shirika hilo limesema, mamlaka husika za Suadia zimewafunga jela kiholela kwa miaka mingi wanaharakati wa haki za binadamu wasiopungua 35 na kuwazuia kusafiri nje ya nchi kwa kosa la kutuma jumbe katika mtandao wa twitter kuhusu kutaka mabadiliko nchini humo.
Licha ya kumalizika hukumu za vifungo za baadhi ya wanaharakati hao lakini mamlaka husika za Saudia bado hazijawaachia huru hadi sasa.