-
Matukio ya Kiislamu Afrika Mashariki na Harith Subeit + Sauti
Dec 21, 2018 23:19Matukio ya Kiislamu wiki hii yamejumuisha masuala mbalimbali ikiwemo kesi ya Masheikh wa Zanzibar wanaoshikiliwa katika korokoro za Tanzania Bara kwa miaka mingi sasa. Harith Subeit na maelezo zaidi...
-
Burundi yakanusha uvumi kuwa inataka kujitoa katika Jumauiya ya Afrika Mashariki + Sauti
Dec 17, 2018 13:43Burundi haijafikiria kujiondoka kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Burundi anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki ambaye amesisitiza kuwa, endapo itabaini kuwa sheria zinakiukwa kwa maanufaa ya baadhi ya wanachama huku wengine wakikandamizwa basi nchi hiyo inaweza kufikiria kuchukua hatua hiyo. HAMIDA ISSA na taarifa zaidi akiripoti kutoka Bujumbura
-
Rais Uhuru Kenyatta aongoza Wakenya katika maadhimisho ya Jamhuri Day + Sauti
Dec 12, 2018 13:27Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Jumatano ya leo amewaongoza Wakenya kuadhimisha miaka 55 ya uhuru wa nchi hiyo (Jamhuri Day) huku maelfu ya raia wakijitokeza katika viwanja mbalimbali nchini humo kuadhimisha siku hii. Saifullah Murtadha mwandishi wetu wa Mombasa ametuandalia ripoti ifuatayo.
-
Wanasiasa wa upinzani Uganda wakutana mjini Kampala + Sauti
Dec 12, 2018 13:22Wanasiasa wa vyama kadhaa nchini Uganda wamekutana katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala katika mjadala maalumu uliogusia masuala muhimu kadhaa ya kijamii na kisiasa kuhusu mustakbali wa nchi hiyo. Kigozi Ismail mwandishi wetu wa Kampala ametuandalia taarifa ifuatayo.
-
Uganda nayo yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu + Sauti
Dec 10, 2018 14:43Uganda imejiunga na nchi nyingine dunia katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Haki za binadamu. Sherehe hiyo imehutubiwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye ametangaza mkakati mpya wa kupambana na ufisadi ambao umeutaja kuwa ni sawa na maradhi ya saratani. Kigozi Ismail na ripoti kamili...
-
Kenya yaorodheshwa kati ya nchi zisizochunga haki za binadamu kwa raia + Sauti
Dec 10, 2018 14:37Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeiorodhesha Kenya miongoni mwa mataifa ambayo hayajazingatia kikamilifu haki za raia wake duniani. Ripoti ya shirika hilo iliyozinduliwa leo Jumatatu imeiorodhesha Idara ya Polisi ya Kenya kuwa inaongoza katika ukiukaji wa haki hizo. Mwandishi wetu wa Kenya, Seifullah Murtadhaa anayo maelezo zaidi...
-
Rais wa Kenya atetea kumteua Moody Awori kuongoza bodi ya hazina ya vijana + Sauti
Dec 08, 2018 14:23Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametetea uamuzi wake wa kumteua Makamu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Moody Awori mwenye umri wa miaka 91 kuongoza bodi ya hazina ya vijana. Maelezo zaidi yamo kwenye ripoti ya mwandishi wetu wa Kenya, Seifullah Murtadha.
-
Shirika la mafuta na gesi la Uganda latambuliwa rasmi kimataifa + Sauti
Dec 03, 2018 23:35Shirika la kwanza la mafuta na gesi la Kigumba, magharibi mwa la Uganda latambuliwa rasmi kimataifa. Mwandishi wetu Kigozi Ismail na maelezo zaidi
-
Tume mpya ya ukweli na maridhiano Burundi yaanza kazi + Sauti
Dec 03, 2018 23:32Mwenyekiti mpya wa tume ya ukweli na maridhiano ya nchini Burundi amekula kiapo mbele ya Rais Piere Nkurunziza wa nchi hiyo. Maelezo zaidi yamo kwenye ripoti ya mwandishi wetu, Hamida Issa...
-
Burundi kuwakusanya watoto wa mitaani "chokoraa" + Sauti
Nov 26, 2018 14:39Ulimwengu unaadhimisha siku ya kimataifa ya watoto wa barabarani, huku serikali ya Burundi ikisema inao mpango wa kuwaondoa watoto wa barabarani katika kipindi kisicho zidi miezi mitatu. Wakati huohuo mashirika ya kimataifa yanakadiria kuwepo watoto wa barabarani zaidi ya elf 3 nchini humo. Kwa maelezo kamili tumtegee sikio mwandishi wetu wa Bujumbura, Hamida Issa...