-
Msaidizi wa Rais Nkurunziza wa Burundi afungwa jela kwa kutoa maneno ya chuki + Sauti
May 01, 2018 02:29Melchiade Nzophabarushe mmoja wa vigogo wa utawala wa Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ametiwa mbaroni na kufungwa jela mjini Bujumbura kwa kutoa maneno ya chuki na ya uchochezi. Mwandishi wetu Hamida Issa na maelezo zaidi...
-
Polisi Uganda wakamata kundi la kigaidi + Sauti
May 01, 2018 01:54Polisi nchini Uganda limenasa kundi jingine la kigaidi linalojihusisha kutoa mafunzo kwa watoto wadogo. Mwandishi wetu Kigozi Ismail ametuandalia ripoti maalumu kutoka Kampala
-
Mzozo baina wazawa na Wachina na watu wenye asili ya Asia wazuka upya nchini Uganda + Sauti
Apr 29, 2018 12:41Mzozo wa kibiashara umezuka upya nchini Uganda ambapo wafanyabiashara wenyeji wanawalalamikia wafanyabiashara kutoka China na India wanaoendesha biashara ndogondogo nchini humo. Mwandishi wetu wa Kampala Kigozi Ismail ametuandalia ripoti maalumu kuhusu suala hilo....
-
Waislamu wenye uwezo wahimizwa kuwasaidia wenzao wasiojiweza hasa wakati wa Ramadhani + Sauti
Apr 26, 2018 12:48Serikali na Waislamu wenye vipato vya juu nchini Kenya wametakiwa kuwasaidia waumini wa dini hiyo tukufu katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan, kama njia ya kuwawezesha kutekeleza ibada ya swaum pasi matatizo. Wito huo umetolewa na viongozi wa kidini huku serikali ikiwa tayari imeondoa ushuru unaotozwa tende zinazo agizwa kutoka ng'ambo kipindi hiki cha matayarisho ya mwezi huo wa neema. Mwandishi wetu Mombasa, Seifullah Murtadha ametutumia ripoti ifuayato.....
-
MINUSCA yafanya uchunguzi kubaini chanzo cha mauaji CAR + Sauti
Apr 26, 2018 12:45Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya kati MINUSCA kimeanzisha uchunguzi katika kata ya Km 5 jijini Bangui ili kujua nini kilifanyika hadi pakatokea mauaji makubwa wakati wa operesheni za kumshika Jenerali Force wa Sungusungu wa kata hiyo. Kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa kilishirikiana na jeshi la taifa katika operesheni hiyo majuma mawili yaliyopita. Mwandishi wetu Mossi Mwassi ana maelezo zaidi...
-
Wadau wa elimu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakutana kujadili changamoto zilizopo + Sauti
Apr 24, 2018 06:32Wadau wa elimu kutoka mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wamesema kwamba tatizo la utofauti wa mitaala na tabia ya wanafunzi kunakiliana kazi wakati wa kuandaa risala zao mwisho wa masomo, ni changamoto kubwa kwenye mfumo mzima wa elimu kwenye nchi hizo. Hii ni kwa kuwa suala hilo limewafanya wanafunzi wengi kukosa utaalamu wa kufaa kuajiriwa kutokana na kutegemea nguvu ya wengine kimasomo. Maelezo zaidi yamo katika ripoti ya mwandishi wetu wa Kigali Sylvanus Karemera.
-
Maafa ya mvua za Masika visiwani Zanzibar + Sauti
Apr 18, 2018 13:36Zaidi ya watu elfu kumi wamekosa makazi visiwani Zanzibar kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha huku nyumba 16 zikipata athari za kuvunjika kuta na kusababisha baadhi watu kuhama makazi yao. Mwandishi wetu Harith Subeit ametuandalia ripoti maalumu kuhusu habari hiyo...
-
Serikali ya Uganda yatakiwa kuheshimu haki za binadamu + Sauti
Apr 18, 2018 13:32Tume ya haki za binadamu nchini Uganda imeshauri vyombo vyote vya serikali kuheshimu haki za washukiwa kwa vyovyote vile. Mwandishi wetu wa Kampala Kigozi Ismail ametuandalia ripoti maalumu kuhusu suala hilo...
-
DRC yataka ipewe fedha zilizokusanywa Uswisi + Sauti
Apr 16, 2018 05:32Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetaka ipewe fedha zilizokusanywa na wafadhili Ijumaa Uswisi ingawa ilisusia kikao hicho. Mossi Mwasi ametuandalia ripoti maalumu kuhusu suala hilo
-
Waislamu Uganda watakiwa kushikamana na dini yao + Sauti
Apr 15, 2018 02:04Waislamu nchini Uganda na duniani kiujumla wametakiwa kushikamana na dini yao kama njia ya kuokoka duniani na Akhera.