Waislamu Uganda watakiwa kushikamana na dini yao + Sauti
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i43122-waislamu_uganda_watakiwa_kushikamana_na_dini_yao_sauti
Waislamu nchini Uganda na duniani kiujumla wametakiwa kushikamana na dini yao kama njia ya kuokoka duniani na Akhera.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 15, 2018 02:04 UTC

Waislamu nchini Uganda na duniani kiujumla wametakiwa kushikamana na dini yao kama njia ya kuokoka duniani na Akhera.

Mwito huo umetolewa na Sheikh Yusuf Mairikit Mulumba mhadhiri wa vyuo vikuu Afrika Mashariki ambaye amesisitiza kuwa walimwengu wanajisababishia wenyewe matatizo kwa kutofuata miongozo ya Mwenyezi Mungu. Amesema hayo katika warsha maalumu ya mafunzo kwa maimamu na viongozi wa Kiislamu mjini Kampala Uganda. Mwandishi wetu Kigozi Ismail amehudhuria warsha hiyo na kutuandalia ripoti maalumu.