-
SEPAH: Malengo matukufu ya ukombozi wa Quds yamekaribia kufikiwa
Sep 29, 2024 06:10Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) ametoa ujumbe maalumu wa pongezi na wa mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon na kusisitiza kuwa, malengo matukufu ya ukombozi wa Quds yamekaribia kufikiwa na historia itathibitisha hilo.
-
Ghalibaf: Sayyid Hassan Nasrullahh ameuawa shahidi katika njia ya ukombozi wa Quds
Sep 29, 2024 06:10Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameuawa shahidi katika njia takatifu ya kuupigania Uislamu na ukombozi wa Quds.
-
Ayatullah Khamenei: Vipigo vya Muqawama dhidi ya utawala unaozidi kunyauka wa Kizayuni vitakuwa shadidi
Sep 29, 2024 02:17Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, akisisitiza kuwa: Njia ya mapambano ya Sayyid wa Muqawama itaendelea na mashambulizi ya Kambi ya Muqawama yatakuwa shadidi zaidi kwenye kiwiliwili kilichochakaa na kinachoeleka kuangamia cha utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Sayyid wa Muqawama; Tangu alipoanza kuwaunga mkono wanyonge hadi kubeba bendera ya Mhimili wa Muqawama
Sep 28, 2024 15:22Sayyid Hassan Nasrullah, ambaye alijulikana kama sayyid wa viongozi wa ulimwengu wa Kiarabu, alipewa jina la Sayyid wa Muqawama na Ukombozi kwa sababu ya msisitizo wake juu ya kanuni na maadili yake katika kuwatetea wanaodhulumiwa na mapambano yake makali dhidi ya ubeberu.
-
Hizbullah yathibitisha: Sayyid Hassan Nasrullah ameuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya Israel
Sep 28, 2024 13:56Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imethibitisha kuwa Katibu Mkuu wa harakati hiyo, Sayyid Hassan Nasrullah, amuawa shahidi katika mashambulizi makubwa ya anga ya Israel yaliyolenga majengo ya makazi ya raia kusini mwa Beirut, jana Ijumaa.
-
Abbas Araghchi: Muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni utaendelea hadi ukombozi wa Palestina
Sep 21, 2024 12:13Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, mapambano na muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni yataendelea hadi ukombozi wa wananchi wa Palestina utakapopatikana.
-
Nasrullah: Adui Mzayuni amevuka mistari yote myekundu
Sep 20, 2024 02:32Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesema maadui wa Kizayuni walivuka mistari yote myekundu siku ya Jumanne kwa kufanya jinai ya kuogofya katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Nasrullah: Operesheni ya kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa Kizayuni ni "Operesheni ya Siku ya Arubaini"
Aug 26, 2024 03:37Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameipa operesheni kubwa iliyotekelezwa na harakati hiyo siku ya Jumapili dhidi ya utawala wa Kizayuni jina la "Operesheni ya Siku ya Arubaini" na kueleza kwamba, ilifanyika kwa mafanikio.
-
Mchambuzi: Nasrullah amedhoofisha uwezo wa kujihami wa Israel
Aug 21, 2024 02:58Mtafiti mmoja wa Kizayuni amekiri uwezo wa Katibu Mkuu wa Hakarati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah na kusisitiza kuwa, kiongozi huyo wa Muqawama wa Lebanon amedhoofisha uwezo wa kuzuia mashambulizi wa utawala wa Kizayuni.
-
Nasrullah: Israel inaogopa majibu ya Iran, Hizbullah kwa jinai zake
Aug 07, 2024 06:52Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema misaada ya nchi za Magharibi kwa Israel ni ithibati kuwa utawala huo wa Kizayuni hauna uwezo wa kujilinda, na unatiwa kiwewe na majibu tarajiwa ya Iran na kambi ya muqawama kwa msururu wa mauaji ya kigaidi uliyoyafanya katika siku za karibu katika eneo.