Abbas Araghchi: Muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni utaendelea hadi ukombozi wa Palestina
(last modified Sat, 21 Sep 2024 12:13:56 GMT )
Sep 21, 2024 12:13 UTC
  • Abbas Araghchi: Muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni utaendelea hadi ukombozi wa Palestina

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, mapambano na muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni yataendelea hadi ukombozi wa wananchi wa Palestina utakapopatikana.

Sayyid Abbas Araghchi amesema hayo katika ujumbe wake kwa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ambapo ametoa salamu za rambirambi kwa kuuawa shahidi Ibrahim Aqeel, kamanda wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon na kusisitiza kwamba, mapambano na jihadi ya muqawama wa Kiislamu Palestina, Lebanon na katika eneo lote la Asia Magharibi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel itaendelea, kwa azma imara zaidi kuliko hapo awali, hadi kukombolewa kwa watu wa Palestina kutoka katika uvamizi na kukaliwa kwa mabavu.

Araghchi amefafanua kuwa jinai za kigaidi za hivi karibuni za utawala wa Kizayuni wa Israel zimethibitisha kwamba utawala huo ghasibu  hauzingatii viwango na kanuni zozote za kimataifa, na uko tayari kufikia malengo yake haramu na ya kivamizi na hata kwa gharama ya kuhatarisha amani na usalama wa eneo.

Shahidi Hajj Ibrahim Aqeel [Hajj Abdul Qader],

 

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuuawa kamanda wake wa ngazi ya juu Ibrahim Aqil katika hujuma ya kigaidi iliyotekelezwa Ijumaa na utawala haramu wa Israe jijini Beirut.

Katika taarifa yake Ijumaa usiku, Hizbullah ilimmiminia sifa tele kamanda wake huyo aliyeuawa shahidi. Taarifa hiyo imesema: "Kiongozi mkubwa wa jihadi, Hajj Ibrahim Aqeel [Hajj Abdul Qader], amejiunga na safu ya ndugu zake waliouawa shahidi, viongozi bingwa waliomtangulia."

Hizbullah imeapa kuendeleza lengo lake la kuikomboa Quds Tukufu hadi  ushindi wa mwisho, Mwenyezi Mungu akipenda."

Tags