-
Makumi ya watu wauawa katika mapigano kaskazini mwa Somalia
Mar 03, 2023 08:40Raia wasiopungua 210 wameuawa katika mapigano yaliyotokea huko Somaliland (eneo linalojitenga kaskazini mwa Somalia), kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya makundi yanayoiunga mkono serikali ya Mogadishu na wapiganaji wanaotaka kujitenga. Mapigano hayo yanaendelea tangu siku 24 zilizopita katika eneo hilo.
-
Umoja wa Afrika waanza kuchunguza chanzo cha kuanguka helikopta ya kikosi chake Somalia
Feb 27, 2023 07:50Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia umetangaza kuanza uchunguzi kuhusu sababu za ajali ya helikopta ya kikosi cha kulinda amani cha umoja huo iliyotokea nchini Somalia.
-
Askari wa jeshi la Kenya waua magaidi wa al-Shabab katika mpaka wa nchi hiyo na Somalia
Feb 17, 2023 03:58Askari wa Jeshi la Ulinzi wa Kenya KDF wamewaua magaidi watatu wa kundi la ukufurishaji la Al-Shabaab la Somalia katika eneo la Sarira kwenye mpaka wa pamoja wa nchi hizo mbili.
-
Jeshi la Somalia latoa pigo jingine kwa al-Shabaab, laua 117 Mudug
Feb 12, 2023 23:04Idadi kubwa ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab wameangamizwa katika operesheni ya jeshi la Somalia katika eneo la Mudug jimboni Galmudug, katikati nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Mapigano yashtadi Somaliland, waliouawa wapindukia 70
Feb 09, 2023 08:35Idadi ya watu waliouawa katika mapigano yanayoendelea kushuhudiwa kwa siku ya nne hii leo katika mji wa Las Anod, mashariki mwa eneo la Somaliland nchini Somalia imeongezeka na kufikia watu 70.
-
Watu 74 wauawa na kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea Somalia
Feb 07, 2023 03:41Watu wapatao 34 wameuawa katika mapigano ya umwagaji damu yaliyotokea kati ya wanajeshi wa Somalia na wanamgambo katika eneo la Somaliland.
-
Kenya na Somalia zakubaliana kushirikiana zaidi ili kuboresha hali ya usalama
Feb 06, 2023 22:56Serikali ya Kenya imetangaza kufungua tena mpaka wa nchi kavu wa nchi hiyo na Somalia kwa lengo la kuboresha hali ya usalama katika mipaka hiyo.
-
Mkutano wa kilele wa Somalia waahidi kuchukua "hatua ya mwisho" ya kulimaliza kundi la Al-Shabaab
Feb 02, 2023 03:53Viongozi wa Somalia na nchi jirani wameahidi katika mkutano wa kilele uliofanyika jana Jumatano katika mji mkuu Somalia, Mogadishu, "kuchukua hatua za mwisho" dhidi ya kundi la Al-Shabaab.
-
Nchi za Afrika kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia kwa ajili ya kupambana na ugaidi
Feb 01, 2023 08:35Serikali ya Somalia imetangaza kuwa imetuma maelfu ya wanajeshi katika nchi jirani kwa ajili ya kupata mafunzo yatakayowawezesha kupambana na kundi la kigaidi la al Shabaab.
-
AU: Tunaridhishwa na mafanikio ya SNA katika vita dhidi ya al-Shabaab
Jan 19, 2023 06:49Umoja wa Afrika umesema kwamba umetiwa matumaini na stratejia inayotumia na Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) katika operesheni zake za kulisambaratisha kundi la kigaidi la al-Shabaab, haswa kwa kutilia maanani mafanikio makubwa liliyoyapata katika kipindi cha wiki moja iliyopita.