-
Jeshi la Somalia laangamiza magaidi 130 wa al-Shabaab
Jun 07, 2021 22:20Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) limetangaza habari ya kufanikiwa kuua wanachama wasiopungua 130 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab katika kipindi cha wiki tatu zilizopita.
-
Amisom kuchunguza kikamilifu madai kwamba KDF inaua raia wa Somalia
Jun 06, 2021 03:25Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) umeahidi kuchunguza madai yanayosema kwamba, Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) limewaua raia katika eneo la Gedo nchini Somalia katika shambulizi la anga dhidi ya wanamgambo wa Al-Shabaab.
-
Somalia yadai jeshi la Kenya linaua raia katika hujuma zake za anga
Jun 05, 2021 21:57Serikali ya Somalia kwa mara nyingine tena imekosoa vikali kile ilichodai kuwa ni tabia ya Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) kuua raia wa Kisomali katika mashambulizi yake ya anga katika eneo la Gedo, jimbo la Jubaland kusini mwa Somalia.
-
Wanachama 30 wa kundi la kigaidi la al-Shabaab waangamizwa na jeshi la Somalia
Jun 02, 2021 02:15Jeshi la Somalia limefanikiwa kuua wanachama wasiopungua 30 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab katikati mwa nchi.
-
Magaidi 100 wa al Shabab wauawa kusini mwa Somalia
May 31, 2021 02:53Jeshi la Somalia limetangaza kuwa, limeua wanamgambo 100 wa genge la kigaidi la al Shabab wakiwemo makamanda kadhaa wa genge hilo katika operesheni maalumu ya kijeshi huko kusini mwa Somalia.
-
Mjumbe wa UN Somalia apongeza mapatano ya viongozi kuhusu uchaguzi
May 28, 2021 22:21Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia James Swan amepongeza uamuzi uliofikiwa na viongozi wa Somalia wa kufanya uchaguzi wa Rais na Bunge ndani ya miezi miwili, ikiwa ni baada ya siku nne za mazungumzo ya kina yaliyofanyika mjini Mogadishu.
-
Somalia kuitisha uchaguzi katika kipindi cha miezi miwili ijayo
May 28, 2021 02:35Serikali ya Somalia imetangaza kuwa sasa uchaguzi mkuu uliokuwa umeakhirishwa kwa miezi kadhaa, utafanyika katika kipindi cha siku 60 zijazo.
-
Watu 6 wauawa katika mripuko wa kigaidi mjini Mogadishu, Somalia
May 11, 2021 03:17Polisi nchini Somalia wametangaza habari ya kuuawa maafisa 6 wa polisi baada ya gaidi mmoja kujiripua kwa bomu katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.
-
AU yamteua rais wa zamani wa Ghana kuwa mjumbe wake Somalia
May 08, 2021 07:58Umoja wa Afrika umemteua aliyekuwa rais wa Ghana, John Dramani Mahama kuwa mjumbe maalumu wa ngazi ya juu wa umoja huo nchini Somalia.
-
Somalia yahuisha uhusiano wake na Kenya baada ya kupita karibu nusu mwaka
May 07, 2021 03:15Somalia imetangaza habari ya kurejesha uhusiano wake na Kenya baada ya kuukata karibu miezi sita iliyopita, ikiituhumu serikali ya Nairobi kuwa inaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.