-
Wasudani waandamana kupinga kuhukumiwa wafanya maandamano
Mar 04, 2019 11:08Maelfu ya wananchi wa Sudan wamefanya maandamano huko Khartoum mji mkuu wa nchi hiyo na katika miiji mingine kadhaa ya nchi hiyo wakitaka kuwa huru mahakama za nchi hiyo na kutowahukumu wafanya maandamano kwa mujibu wa sheria ya hali ya hatari.
-
Middle East Eye: Salah Gosh amefanya mazungumzo ya siri na Israel
Mar 02, 2019 04:36Idara ya Ujasusi ya Sudan imekanusha habari iliyotangazwa na Middle East Eye kwamba mkuu wa idara hiyo, Salah Abdallah Gosh amekutana kwa siri na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Israel MOSSAD, Yossi Cohen.
-
Siku moja baada ya kutangaza hali ya hatari, Al-Bashir ateua Makamu wa Rais na Waziri Mkuu mpya
Feb 23, 2019 23:16Rais Omar al-Bashir wa Sudan ameteua makamu wa kwanza wa rais na waziri mkuu mpya, siku moja baada ya kutangaza hali ya hatari, hatua ambayo haijawa na taathira ya kupoza moto wa maandamano ya mitaani ambayo yameutia msukosuko mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa, utawala wake wa miaka 30.
-
Mabadiliko makubwa nchini Sudan katika kivuli cha mgogoro wa kisiasa
Feb 23, 2019 10:52Rais Omar al Bashir wa Sudan katika hatua ambayo haikutazamiwa amevunja baraza la mawaziri la serikali yake na kutangaza hali ya hatari katika maeneo yote nchini humo. Hatua hiyo imechukuliwa huku Sudan ikiendelea kuzongwa na maandamano yanayomtaka kiongozi huyo ang'atuke madarakani.
-
Rais wa Sudan avunja serikali na kutangaza hali ya hatari 'kuzima' maandamano dhidi yake
Feb 23, 2019 03:09Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan ametangaza hali ya hatari nchi nzima, huku akiipiga kalamu nyekundu serikali ya kifederali ya nchi hiyo.
-
Maandamano yaendelea Sudan, wananchi wamtaka al Bashir ang'atuke
Feb 22, 2019 12:39Askari wa usalama wa Sudan wametumia gesi ya kutoa machozi kukabiliana na mamia ya watu walifanya maandamano leo dhidi ya serikali ya nchi hiyo baada ya Swala ya Ijumaa.
-
Serikali ya Sudan yawakamata viongozi wa upinzani
Feb 21, 2019 12:03Maafisa wa polisi nchini Sudan wamewatia mbaroni viongozi waandamizi wa vyama vya upinzani, muda mfupi kabla ya kuanza wimbi jipya la maandamano dhidi ya serikali.
-
Bunge la Sudan lasimamisha mpango wa kurefusha uongozi wa Rais Bashir
Feb 17, 2019 04:36Kamati ya Bunge la Sudan iliyotwikwa jukumu la kuifanyia marekebisho katiba kwa lengo la kurefusha uongozi wa Rais Omar al-Bashir wa nchi hiyo imesimamisha mpango huo.
-
Sadiq al Mahdi amuonya Rais al Bashir asiendelee kukandamiza waandamanaji Sudan
Feb 11, 2019 10:19Kiongozi wa kambi ya upinzani nchini Sudan ameionya serikali ya Rais Omar al Bashir wa nchi hiyo kuhusiana na hatari ya kuendelea kukandamizwa wananchi wanaoandamana kwa amani.
-
Muungano wa Madaktari Sudan: Watu 57 wameuawa katika maandamano
Feb 10, 2019 09:50Muungano wa Madaktari nchini Sudan umesema, watu 57 wameuawa hadi sasa tangu yalipoanza maandamano ya kupinga serikali tarehe 19 Disemba mwaka jana.