-
Mahasimu Sudan Kusini wahindwa kufikia maufaka kuhusu kugawana madaraka
Jul 20, 2018 09:37Utiwaji saini muafaka wa awali wa amani kati ya rais wa Sudan Kusini na mpinzani wake Riek Machar umeahirishwa, baada ya mahasimu hao kushindwa kuafikiana kuhusu namna ya kugawana madaraka.
-
Rais Salva Kiir: Niko tayari kuunda serikali jumuishi ili kuhitimisha mgogogoro Sudan Kusini
Jul 19, 2018 23:57Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ametangaza kuwa, yuko tayari kuunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayojumuisha pande zote kwa mujibu wa makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya pande husika.
-
Salva Kiir na Riek Machar kutia saini mkataba wa amani Alkhamisi ya kesho
Jul 18, 2018 09:21Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan imetangaza kuwa, pande hasimu nchini Sudan Kusini zimefikia makubaliano ya kugawana madaraka ambayo yatatiwa saini Alkhamisi ya kesho.
-
Baraza la Usalama la UN laiwekea vikwazo Sudan Kusini
Jul 13, 2018 22:51Baraza la Usalama la Umoja wa Umoja wa Mataifa limeiwekea vikwazo vya silaha nchi ya Sudan Kusini, karibu miaka mitano sasa baada ya nchi hiyo kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
-
Upinzani Sudan Kusini wapinga kurefushwa muda wa uongozi wa Kiir
Jul 13, 2018 03:16Saa chache baada ya Bunge la Sudan Kusini kupiga kura na kuunga mkono kurefushwa muda wa Rais Salva Kiir wa nchi hiyo kubakia madarakani hadi mwaka 2021, upinzani unaoongozwa na Riek Machar umejitokeza na kukosoa vikali hatua hiyo.
-
Rais wa Sudan Kusini kuendelea kubakia madarakani hadi 2021
Jul 12, 2018 23:40Bunge la Sudan Kusini Alhamisi limepiga kura kurefusha muda wa rais Salva Kiir kubakia madarakani hadi mwaka 2021.
-
Baraza la Usalama kupasisha vikwazo vya silaha dhidi ya Sudan Kusini
Jul 12, 2018 00:11Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatazamiwa wiki hii kupasisha pendekezo la kuiwekea vikwazo vya silaha Sudan Kusini, siku chache baada ya pande hasimu katika mgogoro wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika kukubaliana kusitisha vita.
-
Raia 232 wameuawa Sudan Kusini miezi miwili iliyopita
Jul 11, 2018 08:57Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limesema raia 232 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa katika maeneo ya Mayendit na Leer nchini Sudan Kusini.
-
SAUTI, Marais Omar Al-Bashir wa Sudan na Yoweri Museven wa Uganda, wamelivalia njuga suala la Sudan Kusini
Jul 09, 2018 11:39Marais Omar al-Bashir wa Sudan na Yoweri Museven wa Uganda, wameongoza mazungumzo ya usuluhishi kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Sudan.
-
Riek Machar kurejeshwa katika nafasi ya Makamu wa Rais wa Sudan Kusini
Jul 08, 2018 03:15Pande hasimu Sudan Kusini zimeafiki kugawana madaraka kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na pande hizo ambapo kwa mujibu wake kiongozi wa waasi nchini humo, Riek Machar atarejeshwa katika wadhifa wa Makamu wa Rais.