-
Jeshi la Syria latungua makombora mawili ya Israel yaliyolenga uwanja wa ndege wa Damascus
Jun 26, 2018 03:02Televisheni ya Syria imetangaza leo kuwa ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimefanya hujuma ya kuushambuliwa kwa makombora Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Damascus.
-
Ndege za kivita za Marekani zawasaidia makamanda wa Daesh Syria
Jun 25, 2018 23:51Ndege za kivita za muungano eti wa kimataifa dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh unaoongozwa na Marekani zimewasafarisha makamanda wawili wa kundi la kigaidi la Daesh kutoka eneo a Tuimin hadi katika kituo cha Marekani kilichoko katika mji wa al Shaddadah mkoani Hasakah nchini Syria.
-
Libya yafurahishwa na uamuzi wa kuanzishwa tena safari za ndege baina yake na Syria
Jun 24, 2018 10:41Waziri wa Uchumi na Viwanda wa Libya amepongeza uamuzi uliotangazwa na Waziri wa Usafiri na Uchukuzi wa Syria kuhusu kuanzishwa tena safari za ndege baina ya nchi hizo mbili.
-
Jeshi la Iraq laangamiza magaidi 45 wa Daesh Syria
Jun 24, 2018 02:37Shambulizi la anga lililotekelezwa na jeshi la Iraq limeangamiza wananchama 45 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika mkoa wa Dayr al-Zawr, mashariki mwa Syria.
-
Assad: Kufanya mazungumzo na Marekani ni kupoteza wakati
Jun 23, 2018 09:27Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema ni kupoteza wakati kufanya mazungumzo na utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu mgogoro katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Syria: Riyadh ingali inawazuia raia wetu kwenda kufanya Hija
Jun 23, 2018 02:55Serikali ya Syria imeukosoa vikali utawala wa Aal-Saud kwa kuingiza siasa katika amali tukufu ya Hija, ambapo Riyadh imewazuia raia wa Syria kwenda kutekeleza ibada hiyo kwa mwaka wa saba mfululizo.
-
Jeshi la Syria lazingira ngome ya jeshi vamizi la Marekani katika mpaka wa Iraq
Jun 22, 2018 09:37Sambamba na operesheni ya kuyasafisha maeneo mapana ya jangwa la Syria, hasa eneo la al-Badiya kutoka mikononi mwa mabaki ya wanachama wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS), jeshi la Syria limezingira ngome ya askari vamizi wa Marekani katika eneo la al-Tanf lililopo katika mpaka wa nchi hiyo na Iraq.
-
Russia yatahadharisha kuhusu njama mpya ya silaha za kemikali Syria
Jun 21, 2018 02:04Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia imetahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea mashambulizi mapya ya silaha za kemikali nchini Syria kwa shabaha ya kuituhumu serikali ya Damascus na baadaye kuishambulia nchi hiyo.
-
Russia yatuma manowari zake mbili zilizobeba makombora ya cruise kwenye pwani ya Syria
Jun 19, 2018 03:06Jeshi la Russia limetangaza kuwa manowari mbili za jeshi hilo zilizobeba makombora aina ya cruise zimetumwa kuelekea bahari ya Mediterania na pwani ya Syria.
-
Tamko la kinagaubaga la Assad; uhusiano wa Iran na Syria haurubuniki
Jun 15, 2018 22:28Rais wa Syria amesema kuhusu pendekezo la Saudi Arabia la kuirubuni nchi hiyo ivunje uhusiano wake na Iran na kuwa tayari kuipatia hongo serikali ya Damascus kwamba: "Si Syria wala si Iran ambayo inatangaza mnada kuhusu uhusiano huu katika soko la kisiasa la kimataifa hata pahitajike mahali pa kufanyia muamala huo."