Ndege za kivita za Marekani zawasaidia makamanda wa Daesh Syria
Ndege za kivita za muungano eti wa kimataifa dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh unaoongozwa na Marekani zimewasafarisha makamanda wawili wa kundi la kigaidi la Daesh kutoka eneo a Tuimin hadi katika kituo cha Marekani kilichoko katika mji wa al Shaddadah mkoani Hasakah nchini Syria.
Duru za ndani ya Syria zimearifu kuwa oapresheni hiyo imefanywa kwa uratibu na ushirikiano baina na vikosi vinavyojiita vya kidemokrasia nchini Syria kwa kusaidiwa na Marekani. Wakati huo huo duru za habari za Wakurdi wa Syria zimeripoti kuwa watu wanne wameuawa katika mapigano kati ya vikosi hivyo vya kidemokrasia vya Syria na kikosi kinachojiita cha wanamapinduzi wa Raqqah wenye mfungano na muuungano wa kidemokrasia wa Syria. Mapigano hayo yalijiri katika mji wa Raqqah huku watu wanne wakijeruhiwa.
Hadi kufikia sasa zaidi ya wanachama 200 kikosi hicho cha wanamapinduzi wa Raqqah akiwemo Abu Issa kamanda wa kikosi hicho wametiwa nguvuni katika viunga vya mji huo.
Duru nyingine ya kijeshi ya Syria imeashiria namna jeshi la nchi hiyo linalovyoendelea kuwaunga mkono raia na kukabiliana kwa pande zote na magaidi wa Jabhatul Nusra na kuripoti kuwa katika hali ambayo makundi yenye silaha tayari yameonyesha nia yao ya kukabidhi silaha; magaidi wa kundi la Jabhatul Nusra wanakwamisha zoezi hilo kwa kuzusha hofu na vitisho.