Assad: Kufanya mazungumzo na Marekani ni kupoteza wakati
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46226-assad_kufanya_mazungumzo_na_marekani_ni_kupoteza_wakati
Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema ni kupoteza wakati kufanya mazungumzo na utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu mgogoro katika nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jun 23, 2018 09:27 UTC
  • Assad: Kufanya mazungumzo na Marekani ni kupoteza wakati

Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema ni kupoteza wakati kufanya mazungumzo na utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu mgogoro katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Katika mahojiano na televisheni ya NTV ya Russia, al-Assad amesema, "mazungumzo na Marekani  hayatakuwa na natija na hivyo ni kupoteza wakati. Hatutafanya mazungumzo na Wamarakeni kwa ajili tu ni Wamarekani." Amesema Syria iko tayarsi kufnaya mazungumzo na wengine ambao kuna uwezekano wa kufikia mapatano lakini hilo haliwezekani na Markeani kwa sababu sera za nchi hiyo hazijabadilika.

Rais wa Syria amesema tatizo la Marekani ni kuwa marais wa nchi hiyo huchukua maamuzi kwa mujibu wa mashinikizo ya taasisi za kifedha na mashirika makubwa.

Rais Trump wa Marekani

Mwezi Mei katika mahojiano mengine Assad alisema tusi la 'hayawani' alilotumia Trump linamaanisha hakika yake (Trump) mwenyewe.

Katika moja ya jumbe alizoandika wakati huo kwenye ukurasa wake wa Twitter, Rais Donald Trump alitumia lugha ya matusi kwa kumwita Rais Bashar Al-Assad wa Syria, 'hayawani'.

Bashar alieleza katika mahojiano hayo kwamba, kuna msingi mmoja maarufu sana unaoeleza kuwa, yanayotoka kinywani mwako yanaakisi vile wewe mwenyewe ulivyo. Kwa hivyo Trump ametaka kuonyesha yeye yukoje, na hilo ni jambo la linalotarajiwa.