-
Serikali ya Tanzania yaahidi kutafuta soko la uhakika la korosho + Sauti
Nov 08, 2018 13:10Serikali ya Tanzania imewataka wananchi hususan wakulima wa korosho nchini humo kuendelea kuwa watulivu wakati ikiendelea kuongea na wanunuzi wakubwa wa korosho kutoka maeneo mbalimbali duniani ili kupata masoko ya uhakika wa zao hilo. Amari Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam...
-
Mchungaji Msigwa: Wafanyabiashara wakubwa nchini Tanzania hawana amani wala uhuru
Nov 07, 2018 04:25Mbunge wa Iringa Mjini nchini Tanzania kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa amesema kuwa, wafanyabiashara wakubwa nchini humo hawana raha wala uhuru wa kufanya biashara ndani ya nchi hiyo.
-
Suitafahamu yaibuka kuhusu kuondoka balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania
Nov 03, 2018 04:47Duru za habari nchini Tanzania zimeeleza kuwa, balozi wa Umoja wa Ulaya nchini humo, Roeland Van de Geer ameondoka nchi hiyo, huku ikielezwa kuwa huwenda amepewa notisi iliyomtaka kuondoka Tanzania.
-
Polisi Tanzania: Waliomteka MO Dewji walihitaji tu fedha; mjadala waendelea mitandaoni
Oct 20, 2018 12:54Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro amesema kuwa, watu waliomteka mfanyabiashara mkubwa wa nchi hiyo na Afrika Mohammed Dewji ‘MO’ walitaka kupewa fedha ingawa hakutaja kiwango hicho cha fedha walichokihitaji.
-
Polisi Tanzania: Tumefanikiwa kupata taarifa muhimu za gari lililohusika katika utekaji wa MO Dewji, Zitto na Lema wapinga
Oct 19, 2018 12:09Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro amesema kuwa polisi ya nchi hiyo imefanikiwa kupata taarifa muhimu juu ya gari lililohusika na tukio la kutekwa nyara mfanyabiashara mkubwa wa Tanzania na Afrika, Mohammed Dewji na kwamba liliingia nchini humo kutoka nchi jirani Septemba Mosi, 2018.
-
Familia ya Mohammed Dewji: Bado hatujapata taarifa yoyote mpya yenye matumaini kuhusu MO
Oct 18, 2018 04:50Familia ya mfanyabiashara mkubwa wa Tanzania na Afrika Mohammed Dewji imesema kuwa, hadi sasa haijapokea taarifa yoyote yenye kutia matumaini ya kupatikana kwa mtoto wao Mohammed Dewji aliyetekwa nyara siku saba silizopita.
-
Serikali ya Tanzania: Hatutoruhusu wachunguzi kutoka nje kuja kuchunguza tukio la kutekwa nyara Mo Dewji
Oct 17, 2018 01:13Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Hamad Masauni amesema kuwa, serikali haiwezi kuruhusu vyombo vya ulinzi na usalama kutoka nje ya nchi kuja kuchunguza tukio la kutekwa nyara mfanyabiashara mkubwa wa nchi hiyo na Afrika Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’.
-
Mbunge Lema: Ili serikali ya Tanzania ijinasue na lawama, iruhusu vyombo vya nje vichunguze kutekwa kwa Mo Dewji
Oct 16, 2018 12:27Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, na mbunge wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, Godbless Lema amesema kuwa njia pekee itakayoiepusha serikali ya Dar es Salaam na lawama kuhusiana na tukio la kutekwa nyara mfanyabiashara mkubwa wa nchi hiyo na Afrika, Mohammed Dewji (MO), ni kuviruhusu vyombo vya nje vifanye uchunguzi wa tukio hilo.
-
Watu 75 watekwa nyara Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu
Oct 13, 2018 12:34Serikali ya Tanzania imesema kuwa, watu wapatano 75 wametekwa nyara katika nyakati na maeneo tofauti nchini humo kwenye kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
-
Licha ya juhudi kubwa za polisi Tanzania, mfanyabiashara mkubwa wa nchi hiyo na Afrika MO Dewji, bado hajapatikana
Oct 13, 2018 04:46Jeshi la polisi nchini Tanzania limeendelea kuwasaka watu waliomteka nyara mfanyabiashara mkubwa wa nchi hiyo na Afrika, Mohammed Dewji, huku juhudi hizo zikiwa bado hazijazaa matunda.