-
Mbunge wa Pakistan mwenye asili ya Tanzania alaani ubaguzi wa rangi Marekani
Jun 28, 2020 03:47Mbunge mmoja wa Pakistan mwenye asili ya Afrika amekosoa vikali vitendo vya utumiaji mabavu na ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa Marekani wenye asili ya Afrika.
-
Binti wa Luther King awataka Wamarekani kuendeleza maandamano ya kupinga ubaguzi
Jun 24, 2020 08:45Binti wa aliyekuwa kiongozi wa harakati ya kupigania haki za kiraia za Wamarekani wenye asili ya Afrika, Martin Luther King, amewataka raia wa nchi hiyo waendeleze maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani hadi uadilifu utakapotendeka.
-
Baraza la Haki la UN lapasisha azimio la kulaani ubaguzi wa rangi
Jun 20, 2020 02:13Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio la kulaani vikali ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi dhidi ya raia weusi katika nchi mbali mbali duniani.
-
Bachelet: Ubaguzi wa rangi nchini Marekani unasikitisha
Jun 18, 2020 03:50Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema anasikitishwa sana na ubaguzi wa rangi wa kimfumo nchini Marekani.
-
Macron apinga kushambuliwa nembo za kikoloni
Jun 15, 2020 22:05Kufuatia kuenea maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi na utaifa huko Marekani ambapo wimbi lake limeenea pia barani Ulaya; wafanya maandamano na wale wote wanaopinga vitendo hivyo vya ubaguzi wameshambulia nembo mbalimbali za kikoloni katika nchi mbalimbali duniani ambazo kwa karne kadhaa zilipelekea raia weusi kutumiwa kama watumwa katika nchi za Magharibi. suala hilo limepingwa na baadhi ya wakuu wa Ulaya akiwemo Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.
-
Kuungana watu wa Ulaya na maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani
Jun 14, 2020 21:53Ukandamizaji na utumiaji mabavu wa polisi ya Marekani dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika licha ya kuwa una historia kongwe, lakini kuuawa Mmarekani mweusi George Floyd jinai iliyofanywa na polisi mweupe katika mji wa Minneapolis kwenye jimbo la Minnesota, sio tu kwamba, kumewasha moto wa malalamiko na maandamano ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika miji mbalimbali ya Marekani, bali malalamiko hayo yameenea hadi katika nchi za bara Ulaya.
-
Masanamu yanayoashiria ubaguzi yaendelea kuvunjwa Marekani na waandamanaji wenye hasira
Jun 12, 2020 03:23Waandamanaji wenye hasira nchini Marekani na maeneo mengine duniani wanaendeleza mkakati wa kuangusha, kuharibu na kuondoa masanamu ya wabaguzi wa rangi.
-
Wananchi wa Senegal waandamana kulaani ubaguzi wa rangi Marekani
Jun 11, 2020 03:34Wananchi wa Senegal wamefanya maandamano kulaani ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi ya Marekani dhidi ya raia weusi wa nchi hiyo.
-
Maelfu wamuomboleza Floyd huku mashinikizo ya kufanyika mageuzi nchini Marekani yakiongezeka
Jun 09, 2020 08:41Maelfu ya waombolezaji nchini Marekani wametoa heshima zao za mwisho kwa George Floyd aliyefia aliyeuawa na polisi, hatua ambayo imeibua maandamano makubwa kote nchini humo dhidi ya vitendo vya utumiaji mabavu na ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa nchi hiyo wenye asili ya Afrika.
-
Malalamiko ya UN dhidi ya ubaguzi wa rangi wa kitaasisi nchini Marekani
Jun 05, 2020 01:27Ubaguzi wa rangi na kizazi na ukandamizaji uliochupa mipaka dhidi ya watu wasio wazungu hasa wenye asili ya Afrika huko Marekani una historia ndefu na ulianza tangu ilipoasisiwa nchi hiyo karne tatu zilizopita. Ubaguzi huo daima umekuwa ni sifa inayochukiza ya jamii ya Marekani. Licha ya Wamarekani wenye asili ya Afrika kuendesha mapambano makali ya kupigania haki zao, lakini hadi leo hii wanaendelea kuwa wahanga wa ubaguzi, ukatili na ukandamizaji usio na kifani.