-
Kuuziwa silaha Saudi Arabia; mwendelezo wa siasa za kindumakuwili za madola ya Ulaya mkabala na vita vya Yemen
Oct 11, 2019 08:51Katika hali ambayo, muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia ungali unaendelea kufanya mauaji huko nchini Yemen, na madola ya Magharibi nayo yameendelea kuiimarisha kijeshi Riyadh kutokana na kuipatia silaha na zana za kijeshi, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amejitoa kimasomaso na kuzitaka Saudia na Imarati kutotumia katika vita vyao huko Yemen silaha zilizotengenezwa nchini Ufaransa kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea kuuawa raia.
-
Sarkozy akabiliwa na kifungo cha mwaka mmoja jela
Oct 03, 2019 00:45Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy anakabiliwa na kifungo na faini iwapo mashtaka yanayomkabili yatathibitishwa na mahakama ya nchi hiyo.
-
Al Sarraj ataka kukomeshwa uingiliaji wa nchi ajinabi huko Libya
Sep 26, 2019 23:08Waziri Mkuu na Mkuu wa baraza la uongozi la serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ametaka kusitishwa uingiliaji wa Imarati, Misri na Ufaransa katika masuala ya ndani ya nchi yake.
-
Hatua mpya za Marekani dhidi ya JCPOA; kupinga mpango wa Ufaransa na kutangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran
Sep 05, 2019 21:55Rais Donald Trump wa Marekani alisikika mara kadha wa kadha akiyakosoa vikali makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, na hatimaye mnamo tarehe 8 Mei, 2018 akatangaza rasmi kujitoa nchi yake katika makubaliano hayo. Kilichofuata baada ya hapo, ilikuwa ni kutekelezwa na serikali ya Trump katika awamu mbili tofauti vikwazo vikali dhidi ya Iran sambamba na kupinga mpango wowote wa kuyalinda makubaliano hayo ya nyuklia.
-
Ripoti ya UN: Marekani, Uingereza na Ufaransa zinahusika kutenda jinai za kivita nchini Yemen
Sep 04, 2019 08:10Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wameandaa orodha ya siri ya watuhumiwa wa kimataifa waliohusika na jinai za kivita nchini Yemen inayoonyesha kuwa Marekani na nchi kadhaa za Ulaya zimehusika pia katika jinai hizo kwa kuuzuia silaha muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia.
-
Amnesty International yaikosoa Ufaransa kwa kuendelea kuziuzia silaha Saudia na Imarati
Sep 01, 2019 08:31Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limeikosoa vikali serikali ya Ufaransa kutokana na hatua yake ya kuendelea kuziuzia silaha Saudi Arabia na Imarati.
-
Rais wa Ufaransa akiri: Kipindi cha ubeberu wa Magharibi kimemalizika
Aug 27, 2019 22:29Rais wa Ufaransa amekiri kuwa kipindi cha ubeberu wa nchi za Magharibi duniani kimefikia tamati.
-
Ukosoaji wa Mkuu wa Baraza Ulaya dhidi ya siasa za kuzusha mizozo za Rais Donald Trump
Aug 26, 2019 03:45Siasa na hatua za Rais Donald Trump wa Marekani katika nyanja mbalimbali hususan kuiondoa Washington katika mikataba na makubaliano ya kimataifa kama ya nyuklia ya JCPOA, mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris Ufaransa na vilevile hatua yake ya kung'ang'ania kuwa na vita vya kibiashara na madola mengine makubwa kiuchumi duniani, ni mambo ambayo yamepelekea kuibuka mizozo mikubwa katika uga wa kimataifa.
-
Rais wa Ufaransa akabidhiwa jukumu la kufikisha ujumbe wa G7 kwa Iran
Aug 25, 2019 08:31Kundi la G7 linaloundwa na madola saba makubwa ya viwanda duniani limemkabidhi Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa jukumu la kufikisha ujumbe na kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Mazungumzo ya viongozi wa Ufaransa na Marekani kuhusu Iran na JCPOA
Aug 25, 2019 08:21Mivutano iliyopo baina ya Marekani na nchi za Ulaya zilizomo katika kundi la 4+1 kuhusiana na jinsi ya kuamiliana na Iran na kadhia nzima ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA bado ni moja ya mivutano mikubwa ya pande hizo mbili. Katika wiki za hivi karibuni, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alifanya mazungumzo mbalimbali na marais wa Iran na Marekani na kuja na mapendekezo ya kupunguza wasiwasi uliopo.