Oct 03, 2019 04:15 UTC
  • Sarkozy akabiliwa na kifungo cha mwaka mmoja jela

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy anakabiliwa na kifungo na faini iwapo mashtaka yanayomkabili yatathibitishwa na mahakama ya nchi hiyo.

Ni baada ya Mahakama Kuu ya Ufaransa kuidhinisha uchunguzi wa faili la kesi ya Sarkozy anayekabiliwa na tuhuma za kutumia "fedha haramu katika kampeni za uchaguzi wa rais mwaka 2012".

Iwapo atapatikana na hatia, rais huyo wa zamani wa Ufaransa atahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na kutozwa faini ya yuro 3750. 

Sarkozy anatuhumiwa kwamba, katika kampeni za uchaguzi wa rais wa mwaka 2012 alitumia kiwango kikubwa cha fedha zaidi ya kile kilichoainishwa na sheria licha ya tahadhari zilizotolewa kwake na vyombo husika. Ushahidi unaonesha kuwa, Nicolas Sarkozy alitumia zaidi ya yuro milioni 20 zinazoruhusiwa katika kampeni za uchaguzi na akatoa mahesabu ya uongo kwa vyombo husika. 

Nicolas Sarkozy

Kesi hiyo pia inawahusisha maafisa wengine 12 wa chama cha Sarkozy. 

Awali Seiful Islam Gaddafi mwana wa kiume wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi alifichua kwamba, baba yake alimpa Sarkozy msaada wa mamilioni kadhaa ya yuro kwa ajili ya kampeni za uchaguzi wa rais.    

Tags