Rais wa Ufaransa akiri: Kipindi cha ubeberu wa Magharibi kimemalizika
Rais wa Ufaransa amekiri kuwa kipindi cha ubeberu wa nchi za Magharibi duniani kimefikia tamati.
Emmanuel Macron aliyasema hayo jana sikku moja baada ya kumalizika mkutano wa G7 katika mji wa Biarritz nchini Ufaransa na kusema kuwa: Umefika wakati kwa Ulaya kufanya jitihada za kujiepusha kutumbukia katika mtego wa vita mpya duniani.
Rais wa Ufaransa ameongeza kuwa, umewadia wakati kwa Ulaya kutazama upya uhusiano wake na Russia na haiwezekani tena kuwaweka Warussi mbali na Ulaya kwa sababu hilo lilikuwa kosa kubwa la kistratijia.
Emmanuel Macron amewaambia mabalozi wa Ufaransa katika nchi za nje kwamba: Mfumo wa uchumi wa dunia umesambaratika kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo kabla, na suala hilo linateteresha mfumo wa kimataifa.
Rais huyo wa Ufaransa amesisitiza kuwa, kwa sasa tunaishi katika zama za mwisho za ubeberu wa Magharibi duniani na maudhui hiyo ilisababishwa na makosa ya nchi za Magharibi katika miaka iliyopita.
Matamshi hayo ya Macron yametolewa baada ya kuongezeka wasiwasi kuhusu sera za kibiashara za Marekani na mivutano iliyopo baina ya nchi hiyo na China.