-
Mkuu wa majeshi Uhispania ajiuzulu kwa kudunga chanjo ya corona bila kuwemo kwenye orodha
Jan 25, 2021 09:04Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Uhispania Jenerali Miguel Angel Villaroya amejiuzulu wadhifa wake kufuatia sakata la kupatiwa chanjo ya corona wakati hayumo kwenye orodha ya watu wenye kipaumbele cha kupatiwa chanjo hiyo.
-
Muuguzi aaga dunia siku 2 baada ya kupewa chanjo ya Covid-19 Ureno
Jan 06, 2021 01:12Maafisa wa afya nchini Ureno wanachunguza kisa cha kufariki dunia ghafla muuguzi mmoja, saa 48 baada ya kupigwa chanjo ya kumkinga dhidi ya virusi vya corona.
-
Mfalme wa zamani wa Uhispania akimbia nchi kwa kashfa ya mlungula wa Saudi Arabia
Aug 04, 2020 03:33Mfalme wa zamani wa Uhispania, Juan Carlos ameondoka nchini humo na kuelekea kusikojulikana wiki kadhaa baada ya kuhusishwa na ufisadi na kashfa ya kupokea mlungula kutoka kwa mfalme wa zamani wa Saudi Arabia.
-
Uhispania yahamisha wanajeshi wake kutoka Iraq na kuwapeleka Kuwait
Jan 09, 2020 08:52Uhispania imewaondoa baadhi ya wanajeshi wake huko Iraq na kuwahamishia Kuwait kufuatia jinai ya karibuni ya Marekani na kushtadi mivutano katika eneo la Asia Magharibi. Uhispania imesema imefanya hivyo kwa kuhofia usalama wa wanajeshi wake.
-
Ghasia zaendelea Barcelona katika maandamano ya watu wa Catalonia
Oct 18, 2019 04:05Ghasia zimeendelea katika mji wa Barcelona nchini Uhispania ambapo Alhamisi jioni migahawa iliteketezwa moto baada ya maelfu kuandamana kwa amani mchana wakitaka viongozi wa eneo linalotaka kujitenga la Catalonia waachiliwe huru.
-
Uhispania yapinga ombi la Marekani la kujiunga na muungano wake wa baharini Ghuba ya Uajemi
Aug 02, 2019 20:55Serikali ya Uhispania imepinga ombi la Washington la kuitaka ijiunge na mungano wake wa baharini katika Ghuba ya Uajemi.
-
Kufichuliwa nafasi ya Marekani katika kusimamishwa meli ya mafuta ya Iran
Jul 05, 2019 02:15Waziri wa Mambo ya Nje wa Hispania amefafanua habari mpya inayohusiana na hatua ya kusimamishwa meli iliyokuwa imebeba mafuta ya Iran katika eneo la Jabal at-Twariq (Gibraltar).
-
Uhispania: Iran haijavunja hata mara moja mapatano ya JCPOA
Jul 03, 2019 22:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa, uamuzi wa hivi karibuni wa Iran haujavunja vipengee vya mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kimsingi hilo ni suala la kiufundi.
-
Uhispania: Kuna uwezekano shambulizi la ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Madrid lilifanywa na Marekani
Mar 11, 2019 04:51Vyombo vya habari nchini Uhispania vimetangaza kwamba, kuna uwezekano vyombo vya intelejensia vya Marekani vilihusika katika shambulizi la siku chache zilizopita dhidi ya ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Madrid.
-
Uhispania yapinga kutumwa nchini Syria wanajeshi wa muungano wa Nato
Feb 17, 2019 23:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania amepinga ombi la Marekani kwa nchi wanachama wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato) kwa ajili ya kutumwa wanajeshi wa nchi hizo huko Syria.