-
Balozi wa Iran UN: Tuhuma za Marekani na Uingereza hazina msingi wowote
Nov 23, 2024 03:51Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekanusha tuhuma dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu zilizotolewa na Marekani na Uingereza za eti kuvuruga amani katika eneo la Asia Magharibi na kuhusika na mapigano yanayoendelea Ukraine; akisisitiza kuwa tuhuma zote hizo hazina msingi wowote.
-
Waingereza waandamana 'Siku ya Balfour' kulaani jinai za Israel Gaza
Nov 03, 2024 02:46Makumi ya maelfu ya watu nchini Uingereza waamemiminika mabarabarani mjini London kushiriki maandamano ya kupinga mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza katika Siku ya Balfour, kumbukizi ya kila mwaka ya kuadhimisha nafasi ya Uingereza katika kuasisiwa utawala wa Kizayuni mwaka 1917.
-
Iran yawaita mabalozi wa UK, Australia mjini Tehran
Sep 04, 2024 03:30Balozi wa Uingereza mjini Tehran ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran na kukabidhiwa malalamiko ya Jamhuri ya Kiislamu, baada ya serikali ya London kuwawekea vikwazo shakhsia watatu Wairan na taasisi moja ya Iran.
-
Iran: Dunia haitasahau nafasi ya UK katika kuundwa utawala wa Kizayuni
Sep 02, 2024 23:38Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, mataifa ya kieneo na dunia kwa ujumla hayatasahau mchango na nafasi ya Uingereza katika kuundwa utawala wa kibaguzi wa Israel katika kitovu cha ulimwengu wa Kiislamu.
-
Iran: Baka la aibu la Mapinduzi ya kijeshi ya 1953 litabakia milele kwenye mapaji ya nyuso za US na UK
Aug 18, 2024 08:45Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, baka la aibu la kuiondoa madarakani Serikali halali ya Iran iliyochaguliwa na wananchi, kupitia mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 28 Mordad 1332 (Agosti 19, 1953) na la kuuhami Udikteta kisiasa, kiusalama na kijeshi litaendelea kubakia milele kwenye mapaji ya nyuso za tawala za Marekani na Uingereza.
-
Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Uingereza ajiuzulu akipinga uuzaji silaha wa nchi hiyo kwa Israel
Aug 17, 2024 22:55Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Uingereza amejiuzulu wadhifa wake katika Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo akipinga uuzaji silaha wa nchi hiyo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Mwanadiplomasia huyo amelaani hatua ya serikali ya London ya kuendelea kuiuzia Israel silaha na kuitaja kuwa haiwezi kuhalalishwa.
-
UN: Maandamano ya kupinga utalii Uhispania yanaweza yakasambaa katika eneo
Aug 12, 2024 07:15Afisa Mkuu wa Mradi wa Utalii Endelevu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO ametahadharisha kuwa maandamano ya kupinga utalii wa halaiki ambayo yameikumba Uhispania hivi majuzi yanaweza yakaenea katika eneo zima.
-
Mamilioni ya wananchi wa Uingereza wapiga kura katika uchaguzi mkuu
Jul 04, 2024 08:41Wananchi wa Uingereza Alkhamisi leo wanapiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kukirejesha madarakani chama kikuu cha upinzani cha Labour, na kumaliza takribani muongo mmoja na nusu wa utawala wa chama cha Conservative.
-
Kiongozi Muadhamu: Israel ilifanya makosa, 'itaadhibiwa' kwa kushambulia ubalozi mdogo wa Iran
Apr 10, 2024 04:22Kiongozi Muadhamu wa wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei anasema utawala wa Kizayuni wa Israel "lazima uadhibiwe na kutiwa adabu" kwa shambulio lake baya dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
-
Corbyn: Kuendelea Uingereza kuipa Israel silaha kunaifanya mshirika katika mauaji ya kimbari Gaza
Apr 01, 2024 07:14Kiongozi wa zamani wa chama cha Labour nchini Uingereza amezikosoa nchi za Magharibi - hasa Marekani na Uingereza - zinazoendelea kuipatia Israel silaha za kuwaua Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na kusema kuwa nchi hizo zinakiuka sheria za kimataifa.