-
Umoja wa Afrika walaani shambulizi la kikatili la Israel dhidi ya hospitali Gaza
Oct 18, 2023 08:55Umoja wa Afrika umelaani vikali shambulio la anga lililofanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya hospitali ya Al Ahli Arab katika Ukanda wa Gaza hapo jana na kuua mamia ya watu.
-
Abdollahian alaani jinai za Israel Gaza: Muda wa utawala wa Kizayuni umemalizika
Oct 18, 2023 08:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kitendo cha Israel cha kushambulia kwa mabomu hospitali na shule katika Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kueleza kuwa: Muda wa kubaki hai utawala wa Kizayuni umemalizika.
-
Balozi wa Israel atimuliwa Colombia kulalamikia jinai za Wazayuni Ukanda wa Ghaza
Oct 17, 2023 02:32Duru mbalimbali za habari zimetangaza usiku wa kuamkia leo Jumanne kwamba, nchi ya Colombia ya Amerika ya Latini imemtimua balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel ikiwa ni kulalamikia jinai za utawala huo dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Ghaza.
-
Abdollahian: Wamagharibi wanapotosha ukweli ili wahalalishe jinai za israel huko Gaza
Oct 14, 2023 04:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi za Magharibi zinafuatilia kupotosha ukweli wa mambo juu ya matukio yanayoshuhudiwa katika Ukanda wa Gaza, ili kwa njia hiyo zihalalishe jinai zinazofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wanaoishi katika eneo hilo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu.
-
Israel yataka wakazi wote wa kaskazini mwa Gaza wahame; imeshaua Wapalestina 1,570
Oct 13, 2023 04:13Utawala wa Kizayuni wa Israel umeuambia Umoja wa Mataifa kuwa, kuna haja kwa wakazi wote wa eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kuondoka na kwenda katika maeneo mengine ya ukanda huo katika kipindi cha saa 24 zijazo.
-
Raisi aitaka jamii ya kimataifa isimamishe jinai za Israel Ukanda Gaza
Oct 11, 2023 23:03Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameikumbusha jamii ya kimataifa kuwa ina wajibu wa kukomesha mgogoro katika wa Ukanda wa Gaza, ambapo Wapalestina wa eneo hilo wanakabililiwa na kila aina ya jinai kutoka kwa Wazayuni.
-
EU: Israel inakanyaga sheria za kimataifa kwa kuiwekea mzingiro Gaza
Oct 11, 2023 08:38Umoja wa Ulaya umesema kuwa utawala wa Israel umekiuka sheria za kimataifa kwa kuuweka Ukanda wa Gaza chini ya mzingiro.
-
UN: Kuiwekea Gaza mzingiro wa kila kitu ni 'marufuku' chini ya sheria za kimataifa
Oct 10, 2023 11:58Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema, mzingiro wa kila kitu ambao Israel imeamua kuuwekea Ukanda wa Gaza, na kuwanyima raia bidhaa muhimu kwa ajili ya maisha, umepigwa marufuku chini ya sheria za kimataifa.
-
Wapalestina wamkumbuka Rachel Corrie, nembo ya mapambano dhidi ya Israel
Mar 17, 2022 05:25Wapalestina wanaadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya mwanaharakati na mwanamapambano dhidi ya utawala haramu wa Israel, Rachel Corrie, aliyeuawa na wanajeshi wa utawala huo ghasibu, kwa kufanya matamasha ya aina mbalimbali na matukio ya michezo.
-
Kukataa utawala wa Kizayuni kushirikiana na Baraza la Haki za Binadamu la UN
Feb 19, 2022 23:22Utawala wa Kizayuni umekataa kushirikiana na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Mwakilishi wa Israel katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa Tel Aviv haitashirikiana na jopokazi la uchunguzi la baraza hilo kwa ajili ya kuchunguza mashambulizi ya mwezi Mei mwaka jana ya utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Ghaza.