-
Borell apendekeza China iwe mpatanishi kati ya Russia na Ukraine
Mar 06, 2022 00:52Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amependekeza nchi ya tatu iwe mpatanishi wa kumaliza mivutano kati ya Russia na Ukraine.
-
Spika wa Bunge la Russia: Rais wa Ukraine amekimbilia Poland
Mar 05, 2022 04:02Spika wa Bunge la Russia maarufu kwa jina la Duma amesema kuwa, Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amekimbilia nchi jirani ya Poland.
-
Khatibu ya Swala ya Ijumaa: Marekani imehusika na yanayoendelea Ukraine
Mar 04, 2022 09:00Khatibu wa Muda wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehrah amekosoa vikali mienendo ghalati ya Marekani katika medani ya kimataifa na kusisitiza kuwa, US ni nembo ya ujahili mamboleo.
-
Maelfu ya Wamarekani wajisajili kwenda kupigana Ukraine
Mar 04, 2022 08:44Maelfu ya wananchi wa Marekani wameuandikia barua ubalozi wa Ukraine mjini Washington wakiomba kuruhusiwa kwenda kupigana na jeshi la Russia wakishirikiana na wanajeshi wa Ukraine.
-
Iran yasisitiza kutumiwa njia ya kisiasa kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Ukraine
Mar 03, 2022 04:41Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kutumiwa njia ya kisiasa kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Ukraine.
-
Russia: Lazima Ukraine ipokonywe silaha na isiwe na nguvu za kijeshi
Mar 03, 2022 03:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema, nchi yake inataka iwepo orodha ya silaha ambazo Ukraine haitaweza katu kuwa na nazo na wala hazitatengenezwa nchini humo.
-
Russia: Tumeangamiza zaidi ya vituo 1,300 vya kijeshi vya Ukraine katika siku ya sita ya vita
Mar 02, 2022 03:51Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa katika siku ya sita ya opereseheni yake ya kijeshi nchini Ukraine imeangamiza vituo zaidi ya 1,300 vya kijeshi vya Ukraine na aina kwa aina ya miundombinu ya kijeshi ya nchi hiyo.
-
Vita vya Ukraine na mabadiliko ya uwiano wa nguvu barani Ulaya
Mar 01, 2022 06:39Kuanza vita vya Russia na Ukraine kumevuruga mlingano wa kijeshi hasa miongoni mwa mataifa ya Ulaya, kiasi kwamba Ujerumani imetenga Euro bilioni 100 kwa ajili ya bajeti yake ya kijeshi, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya mfumo wake wa ulinzi.
-
Kiongozi Muadhamu: Ukraine imekuwa mhanga wa siasa za utawala wa kimafia wa Marekani
Mar 01, 2022 04:45Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Marekani ni utawala wa kimafia na kwamba, Ukraine imekuwa mhanga wa siasa za Washington.
-
Mazungumzo ya Russia na Ukraine yamalizika huko Belarus, haijulikani kama yataendelea au la
Feb 28, 2022 10:22Televisheni ya taifa ya Russia imetangaza kuwa duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya wajumbe wa nchi hiyo na Ukraine imemalizika nchini Belarus, lakini haijafahamika iwapo mazungumzo hayo yataendelea au la.