-
Idadi ya wanajeshi wa kofia bluu majeruhi waongezeka Mali
Feb 11, 2021 04:36Wanajeshi wa kofia bluu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa (MINUSMA) kinachohudumu huko Mali waliojeruhiwa katika mapigano ya karibuni nchini humo imefika 28.
-
UN: Uamuzi wa ICC umefungua mlango wa kupata haki Wapalestina
Feb 10, 2021 20:05Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amesema uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC wa kubariki kuchunguzwa jinai za utawala wa kigaidi wa Israel dhidi ya taifa la Palestina umefungua mlango wa kupata haki Wapalestina.
-
Abdulsalam: Martin Griffiths ni Muingereza katika joho la Umoja wa Mataifa
Feb 10, 2021 04:18Msemaji wa harakati ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah amesema kuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa Yemen, Martin Griffiths, ni Muingereza aliyevaa joho la Umoja wa Mataifa.
-
Iran na Umoja wa Mataifa zajadili mgogoro wa Yemen mjini Tehran
Feb 08, 2021 08:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu inaunga mkono kikamilifu jitihada za Umoja wa Mataifa za kujaribu kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Yemen.
-
Umoja wa Mataifa kuzidisha misaada ya kibinadamu katika eneo la Tirgay, Ethiopia
Feb 07, 2021 23:03Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) umesema kuwa, taasisi hiyo imefikia mapatano na serikali ya Ethiopia kwa ajili ya kuongeza misaada ya kibinadamu katika eneo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo.
-
UN: Hali ya Tigray nchini Ethiopia inatia wasi wasi mkubwa
Feb 05, 2021 09:54Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa, hali ya kibinadamu katika eneo la Tigray huko kaskazini mwa Ethiopia ni ya kutisha mno.
-
Mwakilishi wa UN Somalia alaani vikali shambulio la kigaidi la mjini Mogadishu
Feb 02, 2021 04:01Umoja wa Mataifa nchini Somalia umelaani vikali shambulizi la kigaidi lilofanywa Jumapili kwenye hotel ya Afrika katika mji mkuu Mogadishu na kusababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kusalia majeruhi.
-
UN yakaribisha kuanza kutekelezwa mkataba unaopiga marufuku silaha za nyuklia
Jan 23, 2021 07:27Kuwepo maghala ya silaha za nyuklia duniani na kuongeza na kustawisha pakubwa silaha hizo na pia kujiunga serikali mpya na klabu ya nyuklia kumeibua matarajio yasiyofaa kwa amani na usalama wa kimataifa. Jambo hili limepelekea kutoepukika udharura wa kufikiwa mkataba mpya kwa jina la Mkataba wa Kupiga Marufuku Silaha za Nyuklia yaani The Treaty on the Prohibition of Nuclear Weapons (TPNW) ambao ulipasishwa mwezi Julai mwaka 2017.
-
UN yatoa wito wa kurejeshwa operesheni za uokozi baada ya wahajiri 43 kupoteza maisha
Jan 21, 2021 04:11Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya uhamiaji IOM na lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR yametoa wito kwa nchi kurejesha operesheni za kuwasaka na kuwaokoa watu kwenye bahari ya Mediterania baada ya wahajiri wengine 43 kupoteza maisha katika ajali ya boti iliyotokea siku ya Jumatatu katika pwani ya Libya.
-
Zarif: Mjumbe wa Iran UN hajazungumza na Marekani
Jan 21, 2021 00:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa hajafanya mazungumzo yoyote na Marekani kama lilivyodai gazeti moja la Ufaransa.