Idadi ya wanajeshi wa kofia bluu majeruhi waongezeka Mali
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i66730-idadi_ya_wanajeshi_wa_kofia_bluu_majeruhi_waongezeka_mali
Wanajeshi wa kofia bluu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa (MINUSMA) kinachohudumu huko Mali waliojeruhiwa katika mapigano ya karibuni nchini humo imefika 28.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 11, 2021 04:36 UTC
  • Idadi ya wanajeshi wa kofia bluu majeruhi waongezeka Mali

Wanajeshi wa kofia bluu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa (MINUSMA) kinachohudumu huko Mali waliojeruhiwa katika mapigano ya karibuni nchini humo imefika 28.

Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kuwa, kikosi cha Minusma jana kiliripoti kushambuliwa kambi ya kikosi cha walinda amani hao wa kofia buluu katikati ya Mali. Awali taarifa zilisema kuwa ni wanajeshi 20 wa Minusma ndio waliojeruhiwa katika shamubulio hilo tajwa. 

Maeneo ya katikati mwa Mali yanakabiliwa na hatari ya hujuma za makundi ya wanamgambo wabeba silaha wenye misimamo mikali. 

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) na wanajeshi wa Ufaransa wako nchini humo tangu katikati ya mwaka 2013, hata hivyo wanajeshi hao wamekuwa na utendaji usioridhisha kuweza kudumisha amani na uthabiti nchini humo. Vitisho vya ugaidi pia vinaendelea kushuhudiwa huko Mali licha ya uwepo wa wanajeshi wa Minusma na wa Ufaransa. 

Makundi ya wabeba silaha Mali 

Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasiwasi wake kuhusu kuzidi kuwa mbaya hali ya usalama huko Mali.