Umoja wa Mataifa kuzidisha misaada ya kibinadamu katika eneo la Tirgay, Ethiopia
Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) umesema kuwa, taasisi hiyo imefikia mapatano na serikali ya Ethiopia kwa ajili ya kuongeza misaada ya kibinadamu katika eneo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo.
David Beasley ameandika katika ukurasa wake wa Twitter baada ya kutembelea Mekelle, makao makuu ya Tigray kwamba, serikali ya Ethiopia na WFP zimefikia mapatano kuhusu utekelezaji wa hatua za wazi ili kupanua operesheni za misaada ya kibinadamu katika eneo lote la Tigray. Amesema kuwa Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) hivi karibuni utaanza oparesheni hizo.
Tangu mwezi Novemba mwaka jana serikali la Federali ya Ethiopia inafanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya viongozi wa eneo linalopigania kujitenga la Tigray. WFP imetoa taarifa na kueleza kuwa, imekubali omba la viongozi wa Ethiopia la kutoa misaada ya haraka kwa ajili ya raia milioni moja wanaoishi katika eneo la Tigray.
Waziri wa Amani wa Ethiopia amesema kuwa, serikali imepasisha kwa dharura maombi ya kutumwa askari wa kimataifa katika eneo la Tigray.