Oct 31, 2018 08:23
Mahakama ya Rufaa ya Bahrain imetoa hukumu ya kifo dhidi ya wapinzani wawili wa serikali ya nchi hiyo kwa tuhuma za kuhusika na ugaidi. Mahakama hiyo pia imewahukumu watu wengine 20 hukumu ya vifungo vya baina ya miezi 6 na miaka 25, na wengine 9 wamenyang'anywa uraia.