Oct 18, 2018 07:54 UTC
  • Watoto 30 wanaoshikiliwa na utawala wa Bahrain wadhuriwa na chakula kilichoharibika

Duru za habari nchini Bahrain zimeripoti kwamba utawala wa Aal-Khalifa umewapa chakula kilichoharibika watoto 30 unaowashikilia katika jela huku wasimamizi wake wakikataa kuwapeleka hospitali kwa ajili ya kuwapatia matibabu.

Taasisi ya Bahrain ya Amani kwa ajili ya Demokrasia na Haki za Binaadamu (Peace for Democracy and Human Rights) imetangaza kwamba, taarifa zilizopo zinaonyesha kwamba, jumla ya watoto hao 30 wanaoshikiliwa walilishwa chakula kilichoharibika siku ya Jumatatuu iliyopita, hata hivyo mkuu wa jela ya Houdh al-Jaf alikataa kuwapeleka watoto hao hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mkuu wa jela hiyo alitoa idhini ya kupelekwa hospitali mtoto mmoja pekee kwa sababu tayari alikuwa amezimia.

Maandamano ya amani ya wananchi wa Bahrain ambayo yamekuwa yakijibiwa na ukandamizaji mkubwa wa Aal-Khalifa

Ali al-As'wad mjumbe wa zamani bunge la Bahrain hivi karibuni aliandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba hivi sasa nchi hiyo imegeuka na kuwa eneo la kukanyagwa haki za binaadamu, na kuongeza kuwa utawala wa Aal-Khalifa unazuia kuingia maripota wa haki za binaadamu nchini Bahrain. Tangu tarehe 14 Februaru 2014, Bahrain imekuwa ikishuhudia mapinduzi ya wananchi dhidi ya utawala wa Aal-Khalifa. Wananchi hao wanataka uhuru, kuwepo uadilifu na kuondolewa ubaguzi na kadhalika kuingia madarakani utawala uliochaguliwa na wananchi. Hata hivyo badala ya utawala wa Aal-Khalifa kusikiliza matakwa ya raia wake, uliomba msaada wa askari kutoka Saudia na Imarati kwa ajili ya kufanya ukandamizaji dhidi ya raia hao.

Tags