Aug 28, 2018 03:32 UTC
  • Wananchi wa Bahrain waendelea kupinga siasa za utawala wa Aal Khalifa

Wananchi wa Bahrain wameendelea kufanya maandamano wakipaza sauti za kupinga siasa za utawala wa kifamilia wa Aal Khalifa.

Maandamano hayo makubwa yamefanyika katika kitongoji cha Ma'ameer katika mji mkuu Manama ambapo waandamanaji wakiwa wamebeba mabango na maberamu, wamepiga nara za kulaani siasa za utawala wa Aal Khalifa.

Waandamanaji hao wameapa kuendelzea maandamano yao hadi watakapouondoa madarakani utawala wa kifalme wa nchi hiyo.

Kadhalika wametoa wito wa kuendelezwa harakati za kisiasa na kimapinduzi na kuachiwa wananchi wa Bahrain wajiamulie hatima na mustakabali wa nchi yao.

Tangu  tarehe 14 Februari mwaka 2011 Bahrain imekuwa uwanja wa maandamano ya amani ya wananchi wanaopinga utawala wa kiimla wa ukoo wa Aal Khalifa.

Maandamano ya wananchi wa Bahrain

Wabahrain wanataka magezi katika uga wa kidemokrasia, kama ambavyo pia wanapinga udikteta, utawala na utajiri wa nchi kuwa mikononi mwa watu wachache, kukomeshwa jinai na ukiukwaji wa haki za binaadamu, kukomeshwa ufisadi na uporaji wa mali za taifa na kadhalika wanataka kufanyika mabadiliko katika mfumo wa vyombo vya mahkama.

Pamoja na kuwa matakwa ya wananchi wa Bahrain yako wazi na bayana, lakini watawala wa Manama wamekataa katakata kujibu matakwa hayo na badala yake wamekuwa wakitumia mkono wa chuma na kuwatia mbaroni kiholela wananachi wanaoandamana na viongozi wa upinzani kisha kuwafungulia kesi bandia na kuwahukumu vifungo vya muda mrefu jela kama njia ya kuzima sauti na malalamiko yao.

Tags