HAMAS yatoa shukrani kwa matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi katika Swala ya Ijumaa
(last modified 2024-10-05T12:30:44+00:00 )
Oct 05, 2024 12:30 UTC
  • HAMAS yatoa shukrani kwa matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi katika Swala ya Ijumaa

Mjumbe mmoja wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameshukuru matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika khutba ya Sala ya Ijumaa kwa kutaja oparesheni za makombora za Iran dhidi ya utawala huo katili wa Kizayuni kuwa ni za kihistoria.

Kwa mujibu wa Mtandao wa  al Alam, Mahmoud Mardawi, mmoja wa viongozi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas), amepongeza matamshi ya Ayatullah Ali  Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambaye jana  katika khutba zake kwenye  Sala ya Ijumaa mjini Tehran alisisitiza uungaji mkono madhubuti wa Iran kwa wananchi wa Palestina na Lebanon mkabala wa utawala  wavamizi wa Israel.

Ayatullah Khamenei akiwapungia mkono waumini waliohudhuria Sala ya Ijumaa ya Tehran 04/10/2024

Mardawi amesisitiza juu ya umuhimu wa misimamo hii ya uungaji mkono na engo za kisiasa na kimedani katika kubakia imara na madhubuti taifa la Palestina na Lebanon mkabala wa mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel hasa kwa kuzingatia mashinikizo ya kimataifa na upendeleo wa vikosi vikubwa vya kishetani ambavyo vinafumbia macho mauaji na jinai za Israel katika eneo.

Katika ibada ya kimaanawi na kisiasa ya Sala ya Ijumaa ya jana mjini Tehran, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliashiria sera tofauti za kijeshi, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni za maadui zinazolenga kuleta migawanyiko na akasema, adui wa taifa la Iran ni adui wa mataifa ya Palestina, Lebanon, Misri, Syria, Iraq, Yemen na nchi zingine za Kiislamu na amri zote za kufanya hujuma na kuibua mifarakano zinatolewa kwenye kituo kimoja cha maagizo; na tofauti pekee iliyopo ni mbinu zinazotafautiana zinazotumiwa katika nchi za Kiislamu.

Ayatullah Khamenei alisisitiza kwa kusema, "inatulazimu kufunga mkanda kwa umadhubuti kwa ajili ya ulinzi, uhuru na heshima kuanzia Afghanistan hadi Yemen na kutoka Iran hadi Ukanda wa Gaza na Lebanon katika nchi zote za Kiislamu."

Tags