Hamas: Muqawama utaendelea kukabiliana na mashambulizi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i127816-hamas_muqawama_utaendelea_kukabiliana_na_mashambulizi_ya_israel
Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameonya kuwa kuendelea mashambulizi na hujuma za Israel kunazidisha mapambano na muqawama wa wananchi wa Palestina dhidi ya maghasibu Wazayuni.
(last modified 2025-07-01T12:25:29+00:00 )
Jul 01, 2025 12:25 UTC
  • Usama Hamdan
    Usama Hamdan

Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameonya kuwa kuendelea mashambulizi na hujuma za Israel kunazidisha mapambano na muqawama wa wananchi wa Palestina dhidi ya maghasibu Wazayuni.

Usama Hamdan ambaye ni mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu wa Hamas amesema: Tangu wiki nne zilizopita hadi sasa serikali ya Marekani haijatangaza msimamo wowote wa wazi wa kulaani hatua ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, ya kukataa pendekezo la kusimamisha vita.

Afisa huyo wa ngazi ya juu wa Hamas amesisitiza kuwa katika muda huu wote hakuna ishara yoyote mpya kutoka kwa Wazayuni maghasibu ya kusitisha mashambulizi katika maeneo ya Palestina. 

Hamdan ameongeza kusema: Hamas inaendeleza jitihada za  kufikiwa mapatano ya kusitisha vita na mashambulizi  dhidi ya watu wa Palestina. 

Ameshiria pia kwamba Hamas pamoja na wapatanishi wanafanya juhudi za kufikiwa usitishaji vita na kufunguliwa vivuko ili kuruhusu misaada na  kuboresha hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.