Sheikh Zakzaky aipongeza Iran kwa kuibuka mshindi dhidi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i128010-sheikh_zakzaky_aipongeza_iran_kwa_kuibuka_mshindi_dhidi_ya_israel
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amepongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuichakaza na kuibuka mshindi dhidi ya Israel katika vita vya siku 12.
(last modified 2025-10-17T05:53:46+00:00 )
Jul 06, 2025 14:42 UTC
  • Sheikh Zakzaky aipongeza Iran kwa kuibuka mshindi dhidi ya Israel

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amepongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuichakaza na kuibuka mshindi dhidi ya Israel katika vita vya siku 12.

"Kwanza kabisa, nampongeza Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na watu wa Jamhuri ya Kiislamu, na kwa hakika, umma wote wa Kiislamu kwa ushindi huu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, katika mahojiano na Iran Press.

Matamshi ya kiongozi huyo mashuhuri wa Kishia wa Nigeria yanasisitiza masimulizi ya Iran ya ustahimilivu dhidi ya mashinikizo ya Magharibi na Israel huku yakiangazia umoja adimu kati ya serikali na watu wake katika eneo hilo.

Sheikh Zakzaky ametaja mafanikio ya hivi majuzi ya ulinzi wa Iran, yumkini akimaanisha hujuma iliyozuiwa na uzuiaji wa kijeshi, kama uthibitisho wa Kimungu wa msimamo wake dhidi ya Magharibi. Matamshi yake yanakuja huku kukiwa na taharuki na mvutano mkubwa kati ya Iran na utawala wa Israel.

Ameeleza bayana kuwa, kuishambulia Jamhuri ya Kiislamu ni shambulio kwa taifa zima la Iran kwa sababu wananchi wote wanaiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria katika mahojiano na Iran Press amebainisha kuwa, wachokozi na wavamizi wametumia kila njia kujaribu kuficha kushindwa kwao. Amesema, "Walijaribu kuipiga Iran kupitia upenyezaji na hujuma, lakini wakaambulia patupu.