Askari wapatao 40 wa Israel waangamizwa na kujeruhiwa katika mzingiro Ghaza
(last modified Sat, 05 Jul 2025 07:29:16 GMT )
Jul 05, 2025 07:29 UTC
  • Askari wapatao 40 wa Israel waangamizwa na kujeruhiwa katika mzingiro Ghaza

Kamanda mwandamizi wa Sarayal-Quds, tawi la kijeshi la Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina ametangaza kuwa, askari wapatao 40 wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wameuawa au kujeruhiwa katika operesheni ya kijeshi iliyoratibiwa na wapiganaji wa Muqawama mashariki ya Ghaza.

Kamanda huyo aliyesimamia operesheni hiyo iliyotekelezwa katika eneo la Shujaiya amesema, wapiganaji wa Muqawama walitekeleza kiustadi operesheni ya mzingiro iliyolenga askari wa Israel mashariki ya eneo hilo.

Amebainisha kuwa, askari wa adui walipoteza uwezo wa kujibu mashambulio na kuishia kurudi nyuma tu katika hali ya kuchanganyikiwa huku wakipiga makelele na mayowe bila kujibu mashambulio ya wanamapambano wa Muqawama.

Kamanda huyo wa Sarayal-Quds ameripoti kuwa, wanamuqawama walishuhudia kwa macho yao mabaki ya miili iliyoungua ya maafisa na askari wa jeshi la Kizayuni katika eneo la operesheni hiyo ya mzingiro.

Amesisitiza kuwa, shambulio hilo tata lililofanywa na wapiganaji wa harakati wa Jihadul-Islami ni angalizo rasmi kwamba maghasibu wa Kizayuni, lazima nao pia waonje mateso ya vifo, uharibifu na kubaki bila makazi kama wanavyowafanyia kila mara wananchi madhulumu wa Palestina…/