Sep 06, 2018 07:43 UTC
  • Taasisi ya Haki za Binadamu ya Reprieve: Wabahraini 21 wanakaribia kunyongwa

Taasisi ya Kutetea Haki za Binadamu ya Reprieve jana ilitangaza kuwa Wabahraini 21 ambao wengi ni wafungwa wa kisiasa wanakaribia kunyongwa.

Taasisi hiyo ya haki za binadamu yenye makao yake London Uingereza imewataka viongozi wa utawala wa Aal Khalifa kusitisha haraka utekelezaji wa hukumu hiyo ya kunyongwa kwa raia hao. Taasisi ya haki za binadamu ya Reprieve imeongeza kuwa utawala wa Aal Khalifa  umewatesa raia hao wa Bahrain ili kuwalazimisha kukiri uwongo na imetaka kufanyika uchunguzi kuhusu kufanyiwa mateso na kulazimishwa kukiri raia hao wa Bahrain ambao wengi wao ni wafungwa wa kisiasa. 

Hii ni katika hali ambayo mahakama za kimaonyesho za utawala wa Aal Khalifa hadi sasa zimewahukumu mamia ya wanamapinduzi wa Bahrain kwa tuhuma za uwongo na kisha kuwanyang'anya uraia, kuwanyonga au kuwafunga jela kwa muda mrefu. Harakati za mapinduzi ya wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala wa Aal Khalifa zilianza nchi humo Februari 14 mwaka 2011. 

Nabeel Rajab, Mtetezi mtajika wa haki za binadamu wa Bahrain aliyeko jela

Utawala huo wa Manama umewatia nguvuni viongozi wengi wa upinzani na kuwahukumu vifungo vya muda mrefu jela lengo likiwa ni kuzima mapambano ya wananchi ya kudai haki zao. 

 

Tags