-
Kukosolewa kikao cha mawaziri wa nje wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu, kinachodai kutetea Quds Tukufu
Apr 22, 2022 22:04Katika kikao kilichofanyika Alkhamisi tarehe 21 Aprili huko Jordan, Kamati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiarabu ambayo imepewa jukumu la kukabiliana na hatua zisizo za kisheria za utawala wa kigaidi wa Israel huko Quds Tukufu, imesisitiza udharura wa kusimamishwa mara moja uchokozi na hujuma ya Wazayuni huko Quds na katika Msikiti wa al-Aqsa.
-
Sisitizo la Iran la kurudishwa amani ya kudumu katika eneo kwa kuondolewa ukaliwaji mabavu wa ardhi za Palestina
Apr 22, 2022 03:46Hussein Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa amani ya kudumu katika eneo la Asia Magharibi itapatikana tu kwa kuondolewa kikamilifu ukaliwaji mabavu wa ardhi za Palestina, kurejea wakimbizi wote katika ardhi zao za jadi na kuainishwa mfumo wa utawala wa baadaye wa Palestina kwa msingi wa kura ya maoni pamoja na kuundwa serikali huru katika ardhi hizo.
-
Serikali ya mseto ya Bennett na Lapid katika ncha ya kusambaratika
Apr 21, 2022 21:30Makundi ya Waarabu ndani ya serikali ya sasa ya Tel Aviv yaani United Arab List (UAL) chama kinachowawakilisha Waarabu wanaoishi ndani ya maeneo yaliyotwaliwa na Israel chini ya uenyekiti wa Mansour Abbas mbunge wa Kiarabu ambaye pia ni mwakilishi wa muungano wa serikali ya mseto ya Israel, yametoa masharti kwa ajili ya kubakia katika baraza la mawaziri la Naftali Bennett.
-
Jihad al Islami: Adui Mzayuni anataka kuzusha vita vya kidini
Apr 20, 2022 03:18Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amesema kuwa, adui Mzayuni anafanya njama za kuzusha vita vya kidini katika eneo hili.
-
HAMAS: Muqawama ndiyo njia ya kimsingi zaidi ya kuihami Quds Tukufu
Apr 18, 2022 22:30Mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Baytul Muqaddas ndio mji mkuu wa milele wa Palestina na kusisitiza kuwa, kinachoifanya Quds ibakie ni kuendelezwa muqawama mbele ya adui vamizi.
-
Sisitizo la Jumuiya ya Mwamko wa Kiislamu kuhusu ulazima wa kukabiliana na jinai za Israel
Apr 17, 2022 06:08Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu imetoa taarifa na kulaani hatua za kichokozi na jinai mpya za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina na kusisitiza kuhusu ulazima wa kukabiliana na jinai za utawala huo. Aidha jumuiya hiyo imepongeza muqawama au mapambano ya watu wa Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni.
-
Hizbullah yatangaza mshikamano na wananchi mashujaa wa Palestina
Apr 16, 2022 21:51Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza mshikamano wake na wananchi wa Palestina na kuyatolea wito mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kutekeleza majukumu yao katika kuitetea Quds Tukufu.
-
Russia yaishutumuu Israel kwa kuigeuza Ghaza kuwa jela kubwa ya wazi duniani
Apr 16, 2022 02:48Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imeushutumu utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuligeuza eneo la Ghaza huko Palestina kuwa jela kubwa ya wazi duniani.
-
HAMAS yatoa mwito kwa Wapalestina kusimama imara kukabiliana na Wazayuni
Apr 14, 2022 05:54Naibu wa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema baada ya Wazayuni kuwaua shahidi vijana wanne wa Kipalestina kwamba wananchi wote wa Palestina wanapaswa kusimama imara kupambana kiume na Wazayuni.
-
Al Barghuthi: Jenin haitabaki pekee yake,Wapalestina wataiunga mkono
Apr 14, 2022 02:50Katibu Mkuu wa harakati ya Palestinian Initiative, Mustafa Barghouthi ameeleza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unaoikalia Quds Tukufu kwa mabavu unamwaga daumu za Wapalestina katika juhudi za kuficha kushindwa kwake kisiasa na kiusalama.