-
Idhini mpya ya Uingereza kwa Israel ya kuendeleza mauaji ya umati dhidi ya wananchi wa Palestina
Feb 23, 2024 08:27Uingereza ambayo ni moja ya waungaji mkono wakuu wa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina sambamba na Ujerumani na Marekani, hivi sasa imetoa idhini mpya kwa Israel ya kuendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina hasa wa Ghazza. Madola hayo matatu ya Magharibi ndiyo yaliyoko mstari wa mbele katika kuusheheneza silaha hatari utawala wa Kizayuni ili uzidi kuua raia wa Palestina hasa wanawake na watoto wadogo.
-
Iran: Kuipatia Israel dola bilioni 14 ni sawa na Marekani kutoa bakhshishi kwa mauaji ya Wapalestina
Feb 19, 2024 11:15Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kuidhinishwa na Baraza la Seneti la Marekani msaada wa dola bilioni 14 kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kunaonyesha kuwa Washington inautuza na kuupa bakhshishi utawala huo kwa kuwaua kwa halaiki raia wasio na hatia wa Palestina katika vita visivyo na mlingano vya Gaza.
-
Wanajeshi wa Israel waliovalia sare za madaktari na wauguzi wamewaua shahidi Wapalestina 3 Jenin
Jan 30, 2024 11:29Ripoti kutoka eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan zinaeleza kuwa wanajeshi 10 wa Israel waliokuwa wamevalia sare za madaktari na wauguzi mapema leo Jumanne waliivamia hospitali ya Ibn Sina katika mji wa Jenin na kuwauwa shahidi vijana watatu wa Kipalestina kwa kutumia bunduki zilizowekwa kifaa cha kupunguza mlio wa sauti za risasi.
-
Kuanza kusikilizwa mashtaka ya Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki dhidi ya utawala wa Kizayuni
Jan 12, 2024 02:41Mahakama ya Kimataifa ya Haki yenye makao makuu yake mjini The Hague Uholanzi Alhamisi na Ijumaa inasikiliza na kukusanya mitazamo ya kisheria ya Afrika Kusini na utawala wa Kizayuni kuhusu kesi ya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza. Moja ya shughuli za mahakama hiyo ni kushughulikia mashtaka yanayohusiana na Mkataba wa Mauaji ya Kimbari wa 1948. Mkataba huo unatambuliwa rasmi na nchi 153.
-
Kushindwa Umoja wa Ulaya kuchukua msimamo wa pamoja kuhusu mgogoro wa vita vya Gaza
Dec 16, 2023 11:33Mkutano wa siku mbili wa Baraza la Ulaya umemalizika huku viongozi wa nchi 27 za Ulaya wakishindwa kufikia makubaliano ya pamoja katika taarifa yao ya mwisho kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na matukio ya Gaza.
-
Kushadidi mashinikizo dhidi ya waungaji mkono wa Palestina nchini Marekani
Dec 13, 2023 02:39Marekani ikiwa ni muungaji mkono mkuu wa utawala wa Kizayuni sio tu kwamba, imetoa uungaji mkono mkubwa wa kisiasa na kisilaha kwa utawala huo wakati wa vita vya Gaza, bali mfumo tawala wa Washington pia umeongeza mashinikizo dhidi ya waungaji mkono wa Wapalestina na wakosoaji wa jinai za utawala ghasibu wa Israel.
-
Kura ya veto ya Marekani dhidi ya azimio la Baraza la Usalama kuhusu vita vya Gaza
Dec 09, 2023 11:27Marekani, ambayo ni mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, imepinga azimio lililopendekezwa na UAE la kuanzisha usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.
-
Barua isiyo ya kawaida ya Guterres kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Gaza
Dec 07, 2023 11:58Katika hatua isiyo ya kawaida, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametumia mamlaka aliyopewa kisheria kupitia kifungu cha 99 cha Hati ya Umoja wa Mataifa kulishinikiza Baraza la Usalama la umoja huo lianzishe haraka usitishaji vita huko katika Ukanda wa Gaza.
-
Wito wa Umoja wa Mataifa kuhusu usitishaji vita wa kudumu huko Gaza na onyo la kuenea mapigano
Nov 30, 2023 09:43Siku ya Jumanne, ikiwa ni siku ya tano ya usitishaji vita wa muda huko Gaza, Umoja wa Mataifa ulifanya vikao viwili, kimoja katika Baraza Kuu kuhadili vita kati ya Israel na Hamas na kingine katika Baraza la Usalama kuhusu hali ya Mashariki ya Kati na Syria, ambapo vikao vyote viwili vilizungumzia kuenea mapigano katika eneo na kusisitiza juu ya udhrura wa kutekelezwa usitishaji vita wa kudumu.
-
Ukosolewaji mkali wa undumakuwili wa Magharibi kuhusu kadhia ya Israel na Wapalestina
Nov 21, 2023 07:12Waziri Mkuu wa Ireland, Leo Varadkar amekosoa vikali undumilakuwili wa nchi za Magharibi na kusema kuwa Umoja wa Ulaya na madola ya Magharibi yanashughulikia masuala yanayohusiana na Israel na Palestina kwa undumilakuwili wa wazi.