Wazayuni waendeleza jinai Siku ya Kimataifa ya Quds
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewauwa shahidi Wapalestina wawili kwa kuwapiga risasi.
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni leo Ijumaa sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds wamewafyatulia risasi raia wa Palestina waliokuwepo katika kivuko cha Qalandiya na kisha kuwazuia kuingia katika msikiti wa al Aqsa. Mpalestina mmoja mzee ameuawa shahidi katika ufyatuaji huo wa risasi uliofanywa na wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni.
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni leo hii pia wamemuuwa shahidi kwa kumfyatulia risasi binti mmoja wa Kipalestina katika kituo kimoja cha upekuzi mjini al Khalil karibu na Haram ya Nabii Ibrahim (a.s) katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Aidha wanajeshi katili wa Israel leo asubuhi wameyavamia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ukiwemo mji wa al Khalil na kuwateka nyara Wapalestina wasiopungua ishirini.