Haaretz: Mfumo wa afya ya akili wa Israeli unaelekea kusambaratika
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i106754-haaretz_mfumo_wa_afya_ya_akili_wa_israeli_unaelekea_kusambaratika
Gazeti la Haaretz la Israel limeripoti kuwa wakati mfumo wa afya ya akili wa Israel unakabiliwa na hatari ya kuporomoka, madaktari wa magonjwa ya akili wanaondoka kuelekea Uingereza kutafuta hali bora zaidi ya maisha.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Jan 03, 2024 04:35 UTC
  • Haaretz: Mfumo wa afya ya akili wa Israeli unaelekea kusambaratika

Gazeti la Haaretz la Israel limeripoti kuwa wakati mfumo wa afya ya akili wa Israel unakabiliwa na hatari ya kuporomoka, madaktari wa magonjwa ya akili wanaondoka kuelekea Uingereza kutafuta hali bora zaidi ya maisha.

Gazeti hilo limeongeza kuwa, kugura huko kwa madaktarii wa afya ya akili kunakuja wakati mahitaji ya huduma za afya ya akili huko Israel yanaongezeka kutokana na vita vya Gaza, na kwamba wiki iliyopita wakuu wa vituo vya afya ya akili walituma barua kwa Mdhibiti wa Serikali, Matanyahu Englman, wakionya kwamba "mfumo wa afya ya akili wa Israel unakaribia kusambaratika kabisa.”

Matanyahu Englman

Gazeti hilo lilimnukuu afisa mmoja wa ngazi za juu katika mfumo wa afya ya akili wa Israel ambaye amezungumza na mtaalamu wa magonjwa ya akili akisema: “Kinachowafanya waondoke ni kuchanganyikiwa kutokana na kazi nyingi na kutohisi kwamba hali itaboreka, na kwa kuzingatia hali ya sasa, mzigo wa kazi utaongezeka."

Gazeti hilo liliripoti kuwa mahitaji ya madaktari wa magonjwa ya akili yameongezeka tangu kuzuka kwa vita huko Gaza, na  kwamba "shambulizi la Hamas Oktoba 7 limesababisha takriban wagonjwa 300,000 wa ziada ambao wanahitaji matibabu ya wataalamu."

Wafanyakazi wa sekta ya afya ya Israel pia wametahadharisha kuhusu hatari ya matokeo na athari mbaya za afya ya akili za vita vinavyoendelea Ukanda wa Gaza.