Haniyeh: Israel itawajibika kwa mauaji ya Arouri
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i106756-haniyeh_israel_itawajibika_kwa_mauaji_ya_arouri
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas, Ismail Haniyeh amesema utawala haramu wa Israel utawajibika kwa mauaji ya afisa mkuu wa harakati hiyo, Saleh al-Arouri, na ameyataja mauaji hayo kuwa ni "kitendo cha kigaidi na ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala ya Lebanon."
(last modified 2024-01-03T04:36:49+00:00 )
Jan 03, 2024 04:36 UTC
  • Ismail Haniyeh
    Ismail Haniyeh

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas, Ismail Haniyeh amesema utawala haramu wa Israel utawajibika kwa mauaji ya afisa mkuu wa harakati hiyo, Saleh al-Arouri, na ameyataja mauaji hayo kuwa ni "kitendo cha kigaidi na ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala ya Lebanon."

Haniyeh aliyasema hayo jana Jumanne, muda mfupi baada ya shambulio la kigaidi la ndege zisizo na rubani za Israel dhidi ya kitongoji cha kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut lililoua shahidi watu sita akiwemo Arouri.
"Tunaomboleza mauaji ya shahidi wa kiongozi wa mapambano na mtu mkubwa wa kitaifa, Sheikh Saleh Al-Arouri, pamoja na makamanda wa Al-Qassam, Samir Fandi na Azzam Al-Aqra' na mashahidi wengine, kufuatia shambulizi la kiuoga la Wazayuni huko Beirut", amesema Haniyeh.

Ameongeza kuwa: "Mauaji ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Al-Arouri na ndugu zake ni kitendo cha kigaidi na ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala ya Lebanon, na yanapanua wigo wa uchokozi wake kwa watu wetu na taifa letu."

"Utawala wa Kinazi wa Wazayuni unabeba dhima ya uchokozi huu," aliongeza na kusema: "Damu safi ya Sheikh Saleh al-Arouri na ndugu zake imechanganyika na damu ya makumi ya maelfu ya mashahidi wa Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi, na nje ya nchi."

Saleh al-Arouri

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas ameendelea kusema kwamba "harakati inayowatoa viongozi na waanzilishi wake kama mashahidi kwa ajili ya hadhi na heshima ya watu na taifa letu haitashindwa kamwe."

Mtandao wa televisheni wa al-Mayadeen nchini Lebanon iliripoti jana Jumanne kwamba Saleh al-Arouri aliuawa kufuatia mlipuko uliotokea katika jengo moja katika wilaya ya al-Musharrafieh kusini mwa Beirut.

Arouri ameuawa katika "shambulio la kihaini la Wazayuni," televisheni hiyo imeripoti na kuongeza kuwa, mlipuko huo ulitokea baada ya ndege isiyo na rubani ya Israel kulipua jengo hilo kwa makombora matatu na umeua watu sita.