Ndege za kivita za Israel zaendelea kukiuka usitishwaji vita Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i11224-ndege_za_kivita_za_israel_zaendelea_kukiuka_usitishwaji_vita_ghaza
Ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zimetekeleza hujuma nyingine katika Ukanda wa Ghaza ikiwa ni ukikwaji wa usitishwaji vita katika eneo hilo la Palestina lililo chini ya mzingiro.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 14, 2016 02:09 UTC
  • Ndege za kivita za Israel zaendelea kukiuka usitishwaji vita Ghaza

Ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zimetekeleza hujuma nyingine katika Ukanda wa Ghaza ikiwa ni ukikwaji wa usitishwaji vita katika eneo hilo la Palestina lililo chini ya mzingiro.

Duru zinasema ndege za kivita za Israel, usiku wa kuamkia leo, zimevurumisha makombora mawili katika kijiji cha Juhod ad-Dik kusini mwa Ghaza.

Hakuna taarifa zaidi kuhusu watu kupoteza maisha au mali kuharibiwa katika hujuma hiyo.

Utawala haramu wa Israel mara kwa mara hushambulia kwa mabomu Ukanda wa Ghaza kwa kutumia silaha nzito nzito kinyume cha sheria za kimataifa ambapo aghalabu raia ndio huuawa au kujeruhiwa.

Kwa kushambulia Ghaza, Israel inakiuka mapatano ya usitishwaji vita vyake vya siku 50 dhidi ya Ghaza vilivyomalizika Agosti 26,2014. Katika vita hivyo, Wapalestina karibu 2,200 waliuawa, wakiwemo watoto 577.

Aidha vita hivyo vilisababisha watu zaidi ya 11,100 kujeruhiwa huku kukijiri uharibifu mkubwa katika eneo hilo la Palestina.