Ripoti: Gaza inakabiliwa na hatari kubwa ya njaa
Eneo la Ukanda wa Gaza linakabiliwa na hatari kubwa ya baa la njaa ikiwa ni matokeo ya hujuma na mashambulio ya kinyama ya utawala ghasibu wa Israel.
Shirika linalofuatilia viwango vya njaa duniani, IPC limesema Ukanda wa Gaza unaendelea kukumbwa na hatari kubwa ya njaa, wakati ambapo utawala haramu wa Israel unaendelea kufanya hujuma na mashambulio yake ya kinyama.
IPC imesema katika tathmini yake mpya kuwa, zaidi ya watu 495,000, sawa na zaidi ya humusi (moja ya tano) ya wakaazi wa Gaza, wanakabiliwa na viwango vikali zaidi, vya janga la ukosefu wa chakula.
Shirika hilo limesema, kuongezeka kwa mgao wa ugavi wa chakula na huduma za lishe katika eneo la kaskazini mwa Gaza katika kipindi cha Machi na Aprili ulionekana kupunguza ukali wa njaa katika eneo hilo lililotabiriwa kukumbwa na viwago vikubwa vya njaa.
Wakati huo huo, Mkuu wa Ofisi ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza amesisitiza kuwa njaa inazidi kuongezeka katika keneo kila siku kufuatia kushtadi mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa ukanda huo.
smail al-Thawabateh ameeleza kuwa utawala wa Kizayuni umekiuka sheria za kimataifa kwa kukidhibiti kivuko cha Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza, kukichimba na kukichoma moto. Amesema wagonjwa elfu 25 wameshindwa kutoka Gaza na kwenda nje kwa ajili ya matibabu baada ya utawala wa Kizayuni kukichoma kivuko cha Rafah.