Idadi ya waliouawa shahidi katika Ukanda wa Gaza yafikia 41,000
(last modified 2024-09-09T06:51:44+00:00 )
Sep 09, 2024 06:51 UTC
  • Idadi ya waliouawa shahidi katika Ukanda wa Gaza yafikia 41,000

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, idadi ya waliouawa shahidi kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya eneo hilo imefikia 41,000.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la IRIB, Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, idadi ya wahanga wa mashambulizi ya adui mzayuni Israel kwenye Ukanda wa Gaza imeongezeka na 40,972 waliouawa shahidi na 94,761 elfu waliojeruhiwa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, "katika saa 24 zilizopita, wavamizi wa Kizayuni wamefanya mauaji matatu mapya dhidi ya familia katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha kuuawa shahidi watu 33 na kujeruhiwa 145.

Idadi ya vifo Gaza yapindukia 41,000 baada ya jeshi la Israel kuua Wapalestina wengine wengi

Habari za kuongezeka idadi ya mashahidi na majeruhi katika vita vinavyoendelezwa na utawala huo katili  wa Israel dhidi ya Wapalestina zinatangazwa huku kanali ya habari ya Al Jazeera ikiripoti kuwa: zaidi ya asilimia 70 ya mji wa Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan imeteketezwa na mashambulizi ya kikatili ya utawala haramu  wa Kizayuni.

Matingatinga ya utawala dhalimu wa Israel unaokalia kwa mabavu Palestina yameharibu sehemu kubwa ya mji wa Jenin, ambao ungali umezingirwa kwa zaidi ya wiki moja sasa, na kubomoa barabara na miundombinu mingi ya mji huo.

Wakati huo huo, gazeti la Palestine Post limeripoti kuwa yamefanyika maandamano katika mji wa Nablus ya kuwaunga mkono mateka wa Kipalestina na wakazi wa Ukanda wa Gaza. Halikadhalika, katika maandamano yasiyo na kifani yaliyofanyika huko Tel Aviv, wakosoaji wa Baraza la Mawaziri la Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel Benjamin Netanyahu na waungaji mkono wa makubaliano ya kuwaachilia huru mateka walipambana na wanajeshi.

Ehud Barak, waziri mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni pia amesisitiza kuwa; utawala huo katili wa Kizayuni wa Israel unakaribia kushindwa kuliko kushinda na akafafanua kuwa uamuzi wa kubaki katika mhimili wa Philadelphia wa Ukanda wa Gaza ni mzunguko mtupu ambao hauna uhusiano wowote na uhalisia wa mambo, na kwamba Waziri Mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu ameonywa dhidi ya kubaki katika Ukanda huo wa Gaza kwa muda mrefu.

Tags