Hamas: Kuuawa makamanda wa Hizbullah hakuifanyi Israeli kuwa salama zaidi
(last modified Sun, 29 Sep 2024 02:17:28 GMT )
Sep 29, 2024 02:17 UTC
  • Hamas: Kuuawa makamanda wa Hizbullah hakuifanyi Israeli kuwa salama zaidi

Kufuatia mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Beirut, Hamas imeonya kuwa, hatua hizo hazitaifanya Israel kuwa sehemu salama zaidi.

Shirika la habar la IRNA limeripoti kuwa, kufuatia mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Beirut na kuuawa shahidi baadhi ya makamanda wa Hizbullah, Basem Naim, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas na msemaji wa harakati hyo ametahadharisha kwamba, hatua hizo hazitasambaratisha makundi ya Muqawama wala hazitaifanya Israeli kuwa mahali salama.

Basem Naim 

Basem Naim ameongeza kuwa, Israel inaweza kuwa imepata mafanikio ya kimbinu katika operesheni zake za kijeshi, lakini imefeli katika vita vya kimkakati. 

Matamshi hayo ya msemaji wa Hamas yametolewa baada ya Israel kushambulia makazi ya raia katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut na kuua idadi kubwa ya watu akiwemo Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah, Hassan Nasrullah.