Sep 30, 2024 02:26 UTC
  • Mufti wa Oman: Nasrullah alikuwa mwiba kwenye koo ya Wazayuni

Mufti Mkuu wa Oman amesema Sayyid Hassan Nasrullah, kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon aliyeuawa shahidi karibuni na Israel alikuwa mwiba kwenye koo ya Wazayuni kwa zaidi ya miongo mitatu.

Sheikh Ahmed bin Hamad al-Khalili amenukuliwa akisema hayo na shirika la habari la IRNA na kuongeza kuwa, mrengo wa Muqawama huko Lebanon, Palestina na katika nchi zote za Kiislamu unapaswa kusimama kidete dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Mufti wa Oman amesema anasikitishwa mno na jinai zinazofanywa na jeshi katili la Kizayuni huko Gaza, Lebanon na katika maeneo mengine ya Asia Magharibi.

Mufti wa Oman ameeleza matumaini yake kuwa Waislamu wataungana na kuwa kitu kimoja. Ameeleza bayana kuwa, "Umoja huo utawafanya Waislamu kuwa na nguvu zaidi, kwani maadui wanatumia vibaya mifarakano miongoni mwa Waislamu."

Shahidi Sayyid Nasrullah

Kadhalika Mufti wa Oman ameashiria jinai za utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kusema, pamoja na ukatili na uhalifu unaofanywa na Wazayuni Gaza, lakini tuna matumaini juu ya ushindi mkubwa na wa karibu.

Mwanazuoni huyo wa ngazi za juu zaidi nchini Oman amesema utawala ghasibu wa Israel unajichimbia kaburi kwa vita dhidi ya Gaza na Lebanon, na kwa kufanya uhalifu wa kutisha.

 

Tags