Mufti wa Oman apongeza shambulio dhidi ya makazi ya Netanyahu
(last modified 2024-10-21T06:35:17+00:00 )
Oct 21, 2024 06:35 UTC
  • Mufti wa Oman apongeza shambulio dhidi ya makazi ya Netanyahu

Mufti Mkuu wa utawala wa Kisultani wa Oman amepongeza shambulio la wanamuqawama lililolenga makazi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Kwa mujibu wa ripoti ya IRNA ya leo Jumatatu asubuhi ikinukuu vyombo vya habari vya Kiarabu, Sheikh Ahmad Al-Khalili amesema katika taarifa kwamba, "Kulenga nyumba ya mhalifu na mtenda jinai Benjamin Netanyahu ilikuwa ni hatua ya mafanikio."

Amesisitiza kuwa, "Tunatumai kwamba hatua hii itafanikiwa katika siku zijazo na itatimia. Shambulio hili limetia hofu katika mioyo ya mhalifu huyu [Netanyahu] na marafiki na wasaidizi wake, na Allah akipenda, karibuni hivi litapata tija ambayo utakuwa ushindi wa wazi kwa Muqawama."

Sheikh Al-Khalili amebainisha kuwa, udhaifu wa utawala haramu na mbovu wa Israel umethibitishwa, ingawa wafuasi wake wanaweza kufikiri na kudanganyika kwamba wanaomiliki teknolojia ni bora zaidi na hawawezi kushindwa.

Netanyahu, mtenda jinai za kivita

Vyombo vya habari vya Kizayuni viliripoti Jumamosi kwamba, makazi ya Netanyahu yalilengwa na ndege isiyo na rubani ya Hizbullah na kwamba Netanyahu na mkewe hawakuwapo katika makazi yao huko Kaisaria wakati wa hujuma hiyo.

Mufti wa Oman amekuwa akiunga mkono waziwazi mhimili wa Muqawama ambao umekuwa ukipigana dhidi ya utawala dhalimu wa Kizayuni.

 

 

Tags